Ni ipi mifumo minne inayoisaidia injini kufanya kazi?

Joined
Aug 6, 2023
Posts
31
Reaction score
20
Hellow!

Jaman samahani naomba msaada nimeulizwaa.

Swali kwamba nitaje mifumo minne inayoisaidia injini kufanya kazi!?

Naomba msaada
 
Sijajua kama nitakuwa nimelielewa swali lako, lakini kuna

[emoji419]Mfumo wa mafuta
[emoji419]Mfumo wa umeme
[emoji419]Mfumo wa hewa
[emoji419]Mfumo wa upoozaji


kama unaongelea Strokes za 4 stroke engine kuna

1. Intake stroke - Hapa intake valve inafunguka, piston inashuka chini na mchanganyiko wa mafuta na hewa unaingia kwenye combustion chamber.

2. Compresion stroke - Hapa valves zote zinakuwa zimefunga na piston inapanda juu na kuleta mkandamizo tayari kwa spark plug kuchoma.

3. Power/Combustion stroke - Hapa spark plug inatoa moto na Mchanganyiko wa hewa na mafuta ambao umegandamizwa unachomwa na kuzalisha nguvu kubwa inayoisukuma piston chini.

4. Exhaust stroke - Baada ya piston kusukumwa chini kutokana na mlipuko sasa inapanda juu na exhaust valve inafunguka kuruhusu moshi kusukumwa nje.
 
Kiongoz nakushukulu sanaaa asanteee

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
 
1. Mafuta 2. Ulainishaji 3. Upoozaji 4. Uchomaji..... umeme sio sehemu ya mifumo ndio maana tractor au zile mashine za kusaga nafaka hazitegemei umeme kufanya kazi

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
1. Mafuta 2. Ulainishaji 3. Upoozaji 4. Uchomaji..... umeme sio sehemu ya mifumo ndio maana tractor au zile mashine za kusaga nafaka hazitegemei umeme kufanya kazi

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
Amezungumzia Kwa ujumla

Kwenye mfumo wa muwako (ignition system)

Kuna Vitu kama Hivi

Starter

Alternatol

Na part zingine zilizopo ndan ya Huu mfumo wa umeme

So now days gar Nyingi zimecontain umeme mzee



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…