Yenye mazao mengi, mbao imara na inayokomaa kwa muda mfupi mkuu.
Miti ya mbao inayokomaa kwa haraka mara nyingi hutokana na MBEGU ZILIZOBORESHWA yaani IMPROVED TREE SEEDS lakini kwa uchache sana yaweza kutokana na HALI YA HEWA, HALI YA UDONGO na KIASI CHA MAJI ambacho mti huo wapata.
Kwa mti kuzaa mazao mengi mara nyingi yatokana na AINA YA MBEGU hasahasa IMPROVED TREE SEEDS na BETTER TENDING OPERATIONS (matunzo bora tangu kitaluni [tree nursery] hadi shambani [plantation ])
Lakini pia mazao mengi yaweza tokana na kuusubiria mti hadi ufikie ROTATION AGE (time) yaani KUKOMAA KWA MTI tayari kwa kuvunwa, maana wakulima wengine huvuna miti yao ikingali MICHANGA (immature trees) hiyo hupelekea MAZAO MACHACHE na MBAO DHAIFU/ZISIZO IMARA
Mwisho, MBAO IMARA moja ya sababu ishaainishwa hapo juu na nyingine ni kuwa na BETTER TREE NURSERY MANAGEMENT & TENDING OPERATIONS ( usimamizi bora wa kitalu cha miti na shamba la miti) bila kusahau AINA YA MTI (tree species)
Kwa ushauri zaidi waone
a)WAKALA WA MBEGU WA TAIFA (Tanzania Tree Seeds Agency - TTSA)
b)TAASISI YA UTAFITI WA MISITU TANZANIA (Tanzania Forestry Research Institute- TAFORI)
c)TAASISI YA UENDELEZAJI MISITU (Forestry Development Trust-FDT)
d)MPANGO WA UPANDAJI MITI (Private Forestry Programme-PFP)
Note: Taasisi mbili za mwanzo (TTSA na TAFORI) ni TAASISI ZA TAIFA na mbili za mwisho (FDT na PFP) ni TAASISI ZA KIGENI