Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Hakika hawa wanawake wawili ni watu muhimu sana katika maisha ya mume, lakini kila mmoja mara nyingi huwa anahitaji kuwa chaguo la kwanza, na hapo ndipo shida inapoanzia.
Nadhani mara nyingi tumeshawahi shuhudia ima kwa majirani au kwa ndugu zetu,jinsi wanawake hawa muhimu wanavyo chachafya ndoa nyingi.
Na wakati mwingine tumeshawahi kuona katika clip au video mbali mbali,jinsi wakati mwingine wanawake hawa ambao ni vipenzi kwa mume, wakigombea kukaa sita ya mbele kwenye gari. Inaweza isiwe hivyo katika picha halisi, lakini inaonyesha jinsi wanawake hawa wanavyoweza kuwa paka na panya katika maisha ya mwanaume.
Maana mama anaona anastahili kupata mema ya mwanae kama mzazi,na huku mke anaona anastahili kupata mema kama kipenzi na tamu ya mume.
Sasa mwanaume hapa unatakiwa uwe na busara na hekima kubwa sana,hutakiwi kuwaonyesha mbele yao,nani ana hadhi kubwa kuliko mwingine, ila ukiwa na mmoja wao kwa wakati wake muonyeshe yeye ndio kila kitu kwako.
Yaani unatakiwa uwe na akili kubwa ya kudili na hawa wanawake muhimu katika maisha yako,natambua mama ndio kila kitu,lakini kumbuka hata mkeo nae ana nafasi yake, sikwambii kwamba umpe kipaumbele mke kuliko mama laa! Ila usimfanye akaona wazi kuwa yeye hana thamani kwako.
Lingine hili lipo kidini zaidi,usimnyanyase mke kwa ajili ya mama yako, yaani iko hivi, majukumu ya mama yako ni yako na si ya mke, yaani isifike kipindi mke akaona kero kwa kuwa unamshinikiza sana amjali mama yako,ingawa kihekima na busara huyo ni mama yake pia,lakini kiuhalisia ana mama yake huko kwao
Na wakwe najua kuna baadhi yenu mko humu,sio busara kuingilia ndoa za watoto wenu kisa tu wewe ndio ulimzaa huyo mtoto wa kiume ambaye ni mume wa mkweo, maana kuna ile kauli "je nisingemzaa ungempata huyo?" Wewe ulishamzaa basi inatosha, waache wengine wamtumie.
Na wake nanyi, sio kwasababu huyo mume ndio tamu yako,basi ukajisahau na kuona huyo mumeo hana mama, tambua kama unavyo mthamini mama yako, mumeo nae anamthamini mama yake vile vile, kwahiyo msitake kuchukua nafasi ya mama yake, hamtaweza abadani.
Nawaaibia siri ila msimwambie mtu! Jipendekeze kwa mama wa mumeo hata kinafiki,kwanza mama atakupenda, na mume pia atakupenda.
Ni hayo tu!