Ni ipi tafsiri ya neno Mganga Mfawidhi?

Ni ipi tafsiri ya neno Mganga Mfawidhi?

Xavier Wenger

Member
Joined
Nov 11, 2021
Posts
11
Reaction score
17
Ndugu zangu wana JF naomba msaada nataka kujua maana ya neno au tafsiri ya neno Mganga Mfawidhi kwa kiingereza.

Asante
 
Mfawidhi maane yake ni kiongozi wa sehemu hiyo; hayo ni madaraka. Hakimu mfawidhi ndiye hakimu anayeongoza mahakimu wengine kwenye mahakama husika. Mganga mfawidhi ni Mganga anyeongoza waganga wengine katika taasisis husika. Kiingereza chake is Medical Officer In Charge, hiyo ni tofauti na Chief Medical Officer ambayo ni ngazi kwenye msululu wa vyeo vya waganga. Hospitali inaweza kuwa na chief medical officers kadhaa lakini ni mmoja tu ndiye in charge
 
Na je mtu akiitwa mchawi mfawidhi (jokes)
 
Medical officer Incharge
huyu ndiyo mtendaji mkuu wa hospital/Kituo cha Afya.
Anafanya mambo yote ya technical yawe mahala pake
DMO yeye ni mtawala tu. hupata namna huduma zinavyoenda kutoka kwa huyu M/I
 
Back
Top Bottom