Ni Jambo Gani Bado Unalidumisha Linalohusu Ukoo Wako?

Ni Jambo Gani Bado Unalidumisha Linalohusu Ukoo Wako?

holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
1,859
Reaction score
2,986
Wakuu,
Licha ya kuwa asilimia kubwa ya watu wameacha tamaduni na mila zao za asili kwa utetezi kwamba zimepitwa na wakati.

Lakini kuna msemo wa wahenga unasema mtu haachi asili yake,hata wewe kuna jambo bado unalidumisha hata kama maisha yako yametawaliwa na usasa na mambo leo.
Kwa upande wangu siwezi kuacha kufanya matambiko, nikipatwa na shida yeyote,lazima niende kwenye makaburi ya ukoo wangu,nikapalilie majani,niongee shida zangu, shida zikiisha nitaamini nimesaidiwa na mizimu ya wahenga wangu,japo mimi ni muumini wa kiongozi wa dini fulani (staitaja).

Wewe unafkiri ni kautamaduni gani hutaki kukaacha?

Tiririka.
 
Nadumisha ufugaji wa sharafa kama Carl Peter.
Screenshot_2025-02-22_181305.jpg
 
Huwezi kula mtu anakuangalia ni mwiko, hata kama kashiba lazima ale.

Mgeni lazima akaribishwe vizuri, lazima achinjiwe, kuku,mbuzi au hata mjusi.
 
Huwezi kula mtu anakuangalia ni mwiko, hata kama kashiba lazima ale.

Mgeni lazima akaribishwe vizuri, lazima achinjiwe, kuku,mbuzi au hata mjusi.
kwenye mjusi umetupiga mkuu!
 
Kuwa mkarimu kwa ndugu sisi ukoo wetu ni marufuku ndugu kufikia Lodge akiwa mkoa fulani kikazi n.k even wanafunzi wa chuo, n.k wanakaa kwa ndugu yoyote tu bila shida no need ya kukaa hostel.

I’m proud to be part of this clan tunaishi kwa upendo mkuu sana.
 
safi sana mkuu
 
Baada ya kukutana na mamia ya watoto wa wazungu na kugundua hakuna hata mmoja anayeitwa masawe wala Otieno, nimeamua kuwapa wanangu majina ya kwao, wawe na utambulisho unaoendana nao badala ya kufeki majina ya tamaduni za watu.
safi sana mkuu!
 
Back
Top Bottom