Clever505
JF-Expert Member
- Jul 27, 2020
- 1,183
- 2,256
Habari zenu wanaJF!
Ni hivi, kuna msichana mmoja nilizoeana nae sana kipindi alipokuwa ameolewa. Kuna kipindi ndoa yao iliingia dosari akaachana na mumewe wakiwa na mtoto mmoja, kiufupi huyu msichana hakuwa na kosa la kuachwa Ila mumewe alifanya maamuzi haraka sana ya kumuacha kwa mambo ya kuambiwa.
Sasa huyu msichana akawa anafarijika sana akipiga nami stori ikafikia muda akataka tuwe wapenzi. Hilo jambo kwangu lilikuwa gumu kwa sababu mumewe tulikuwa tunaheshimiana sana kwa hivyo nikawa naona haitakuwa poa endapo itasikika mi nipo na mama wa mtoto wake japo wameachana. Sisi wanaume ni ngumu sana kumkataa msichana anaposema anakuhitaji, kwa hiyo nikajikuta nakubali tuwe wapenzi na tukakubaliana iwe siri sana asijue mtu yeyote. Kwa usiri tulifanikiwa maana hadi sasa hakuna anayejua.
Ni msichana ambaye amenizidi umri, alishawahi kuniambia kwamba kabla hajaolewa alishawahi kutongozwa na bro wangu ila alimkataa. Ila kwa sasa bro anamtaka tena baada ya kuona huyu msichana hayupo kwenye ndoa yake ila bado anagonga mwamba kwa sababu mi ndo nipo nae na hakuna anayejua.
Sasa kilichonifanya nije hapa kuandika hii habari yangu ni kwamba, mara kwa mara huyu msichana anaongelea sana swala la yeye kuhitaji sana mtoto mwingine, yaani anataka kuzaa mtoto wa pili. Kiukweli mi sipo tayari kwa hilo, na mara zote huwa nikisex nae huwa namwaga nje maana kutumia ndom ni kitu ambacho yeye hataki kabisa.
Jambo ambalo naomba msaada wa mawazo kwenu ni kwamba, mwezi wa5 mwaka huu alikuja geto amekaa siku mbili na kila tuliponyanduana nilikuwa makini sana sperms lazima zimwagwe nje. Alipoondoka, siku chache mbeleni akaniambia kwamba ana mimba yangu...Nikawa mpole kidogo, nikamkumbusha vile huwa namwambia kuhusu mimi kutokuhitaji mtoto, nikamkumbusha pia na juhudi zangu nilizokuwa nazifanya za kumwaga nje, akaelewa wazi kwamba mi sihitaji mtoto ila sio kwamba nimekataa mimba. Na nilionyesha kumpenda sana japo amebeba mimba bila makubaliano. Mi nikajua wazi kwamba ameibeba kwa makusudi tu japo sielewi imeingiaje wakati mara zote namwaga nje.
Alilia Sana baada ya mi kujitetea sana juu ya mimba aliyonayo japo sijaikataa...mwisho wa maongezi yetu siku hiyo akasema kwamba alikuwa ananitania tu na hana mimba. Kesho yake akanihakikishia kwamba alikuwa ananitania na nikaamini kwamba kweli amenitania japo nilibaki na wasiwasi maana kile kilio kilikuwa kizito na si cha kuigiza. Nikajua ni lazima anayo na ataitoa kwa Siri bila mi kujua.
Sasa jana tena amesema mimba anayo nilipoanza kumuhoji aniambie ukweli kabisa asinizungushezungushe akabadilisha na kusema hana. Nimemhakikishia kwamba, namlaumu kwa kupata mimba bila makubaliano na mimi ila siikatai; akasema anatania.
Hadi sasa nahisi anayo ila hataki kusema ukweli. Sasa nawaza, kwa kuwa sikai nae mkoa mmoja itakuwaje akiendelea kukaa kimya kisha akaja ghafla kunipa taarifa kwamba ana mtoto wangu? Bro wangu anajua sana kwamba mi naelewa kuwa anamtaka na alitaka kabisa kumuoa, itakuwaje akigundua yule msichana ana mtoto wangu! Watu mtaani walijua sana vile mi nilimheshimu huyu msichana pamoja na mumewe, watanionaje wakiona nimempa mimba?
Nisaidieni mawazo hapo. Naongeza kitu kingine kidogo, siku aliponiambia ana mimba nilipoonekana kutopenda jambo hilo akasema nisiwe na wasiwasi na kuhofia kuilea mimba kwa sababu atailea mwenyewe. Akasema tena, kama sitahitaji kujulikana nimuachie mwenyewe jambo hilo atajua mwenyewe jinsi atakavyoliwasilisha kwao bila uhusika wangu. Sasa Nina hofu anaweza kufanya hivo kwamba akazaa na asinihusishe kwa chochote.
Samahanini kwa maelezo marefu ndugu zangu.