Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Ni matumaini yangu nyote ni wazima na wenye Afya tele. Afya ya mwili ni muhimu sana kwa afya ya akili. Binadamu hatoweza kufikiri vizuri kama Afya yake mwili haiko sawa sawa.
Kwahiyo ndugu zangu ni muhimu sana kuangalia Afya zetu ili kuweka imara akili zetu siku zote, na kufanya miili yetu kuwa yenye kuchangamka.
Bila akili iliyo imara hatutaweza kuendesha maisha yetu ya kila siku hapa duniani. Ni akili pekee zinazotufanya tuendeshe maisha yetu ya kila siku na miili yetu inatusaidia tu kufuata kile akili inachotaka.
Tufanye pia akili zetu ziwe active wakati wote ili miili yetu ipate kuwa yenye rutuba. Tulinde na tuelekeze akili zetu kwenye mambo yenye manufaa kwa taifa letu, kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii nzima.
Kwahiyo ndugu zangu tuondoe hofu kuhusu maisha ili tuweze kuishi kwa ukamilifu katika hii dunia kwasababu hofu huondoa furaha ya binadamu.
Binadamu tunapokuwa na hofu tunashindwa kufikiri sawa sawa basi tuondoe uwoga na hofu na tujiamini na tuwe na matumaini na kesho. Tupange mipango yetu kwa uhakika na kwa fokra sahihi tukitumaini kesho itakuwa bora zaidi.
Tujiulize swali hili muhimu ni nani anayejua baadae yake au aliyewahi kuiona kesho? Kesho kuna giza hakuna mtu mwenye uwezo wa kuiona kesho yake itafananaje. Kwahiyo tuishi maisha ya leo kwa ukamilifu wake tusihofu kuhusu kesho.
Hili ni neno muhimu sana kwenu ndugu zangu. Tuishi maisha ya leo kwa ukamilifu wake. Kwasababu hakuna aliyewahi kuishi kesho wote tunaishi leo.
Maisha yetu hapa duniani yanaenda kwa kasi ya ajabu mno. Tunazaliwa, tunakua tunakufa. Lakini kitu kimoja ambacho ni muhimu kwa binadamu yeyote aliye hai ni Matumaini.
Matumaini moyoni mwa binadamu ni kama mafuta kwenye gari. Ili binadamu aishi ni lazima awe na matumaini. Ndugu zangu mioyo yetu lazima ijawe na matumaini na upendo. Ni muhimu kujifunza kuwanyanyua wale waliokata tamaa. Kwenye matumaini kuna maisha.
Nakumbana na hali ngumu kila wakati katika safari yangu lakini kitu kimoja na muhimu kinachofanya niendelee ni matumaini.
Tuna struggle yes, lakini matumaini ndio mafuta yetu kama petroli kwenye gari na tunaamini iko siku yale yote tunayotumaini yatakamilika. Yes there is hope! We can stand up today na kupiga kelele kuna matumaini.
Naongea hili kwa mtu mmoja mmoja na kwa nchi. If we stand together today as a country with the hope and courage na tukiwa na dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko katika taifa letu kwanini tusiweze?
Tumegawanyika kama nchi hili liko dhahiri, na kwa kugawanyika kwetu hatutaweza kufikia malengo. HATUTAWEZA kuvuka daraja na kupambana na adui katika mgawanyiko huu katika nchi. Hili ni kweli kwa kugawanyika kwetu tunadhoofisha nguvu yetu kama NCHI.
Nchi hii inahitaji uongozi sasa hivi, ili kuleta watu wa taifa hili pamoja na kuunda dira itakayotutoa hapa tulipo. Hatuwezi kuendelea kuwa na viongozi waliokosa Courage na Determination ya kuliondoa taifa hapa lilipo.
Nitaendelea kuamini na ninaamini nchi hii haijaumbwa kuwa ya mwisho ina uwezo wa kuwa kubwa.
Kuna vitu viwili tu hapa; tuamini kama tuna uwezo huo na kufanya jitihada na maarifa kufikia ndoto hiyo au tusiamini tubaki tulivyo?
Sisi kama nchi ni lazima tuamue kwa dhati kabisa ni wapi tunataka kwenda au tuendelee kukwama tulipo ambapo hakuna taifa linalotutambua duniani wala kutuheshimu?
Naamini ni lazima tuibuke kileleni. Tuna nguvu hiyo. Lakini hii ni safari sio ya siku moja au mbili ni safari ya vizazi kufanya juhudi zisizo fifia katika maarifa na ujenzi wa taifa hili.
Ni lazima tuanze sasa na tuwatayarishe vijana wetu kwa hii safari. Kama tunataka heshima kama taifa ni lazima tufanye hili. Tujiulize ni nguvu kiasi gani tunatumia kila siku katika ujenzi wa taifa hili? Tujiulize je tuna dhamira ya dhati ya kulitoa taifa hapa lilipo?
Hiki kitu kinahitaji commitment na watu waliojitoa wasiogopa kifo bali kukamilisha dhamira ya kulifanya taifa hili kuwa kubwa na hiyo ndio ndoto yao ya kila siku.
Mawazo wa vijana wetu wa sasa hayawezi kulifikisha taifa hili tunapopataka tunahitaji kubadilika. Heshima yetu itakuwepo tutakaponyanyua taifa hili kuwa kubwa na raia wetu kutambulika popote watakapo kwenda na kuheshimiwa.
Hili ni jambo linalowezekana , lakini viongozi vibaraka wa Afrika wanaogopa kuwaambia. Wanaogopa kuwaambia mnauwezo wa kuyafanya mataifa yenu makubwa, nguvu hiyo iko mikononi mwenu kama mkitia juhudi wanaogopa struggle.
Wazungu ni binadamu kama sisi wakati umefika sasa wa kufanya kizazi chetu kinyanyuke kutoka katika usingizi wake. Na kujifunza kutoka katika historia ya kutawaliwa na kuamua sasa kujenga umoja katika taifa letu na kulifanya taifa letu kujitegemea hili linawezekana kama tukifanya kazi kwa pamoja. Na kwa kushirikiana.
Tuwaache watu wenye uwezo wa kuongoza washike taifa hili, ili kuleta heshima na maendeleo ambayo taifa hili linahitaji. Tusitake uongozi kwa faida binafsi tutaliua taifa hili.
Mtu yeyote mwenye akili anaona taifa letu lilipofikia. Anaona umoja wa watu wetu ulivyoyumba, anaona uzalendo ulivyoshuka na anajua nchi hii inahitaji matibabu.
Anajua taifa hili limekosa malengo ya pamoja liko katika confusion. Watu wataifa hili wengi hawajitambui kuhusu utaifa wao. Tunahitaji kujenga utaifa.
Tusikubali kitu kinachoitwa globalization kuua utaifa wetu, kuua uzalendo wetu na jitihada zetu kulifanya taifa hili kubwa. Tuna haki ya self preservation and growth. Tusikubali kuua identity yetu kama waafrika na kama watanzania. Tusikubali dissolution of our culture and our values.
Ni wakati sasa kuvifanya vyuo vyetu kuwa active na vya watu wanaofikiri sio kiwanda cha kuzalisha waajiliwa. Hili ni muhimu sana. Hatutaweza kuendelea kama hatutakuwa na vijana wanaofikiri sawa sawa na ambao ni responsible.
Tunahitaji kujenga committed citizens not just citizens. Na vyuo vyetu viwe pale ku serve jamii zetu na taifa letu. Kuzalisha vijana ambao watakuwa tayari kujitolea kwa ujenzi wa taifa hili.
Wakati ni huu hatuna wakati mwingine kulifanya taifa hili kubwa. Ni jambo linalowezekana na liko chini ya uwezo wetu wa kibinadamu. Tunaweza sasa kuwafundisha vijana wetu umuhimu wa taifa hili kwao. Tukianzia katika ngazi ya familia kwa kuzijenga kuwa imara na za kizalendo na jamii zetu kutambua umuhimu wa taifa hili kwa maisha yao ya kila siku.