Ni jini au nini?

Ni jini au nini?

utafiti

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Posts
12,783
Reaction score
7,667
Habari wana jf, poleni kwa kazi kubwa ya ujezi wa taifa, nina rafiki yangu wakaribu sana (mwanamke) anatatizo la kuota ndoto mbaya, anaweza kuota kama sauti inamwita kwa jina lake nje tena hua anatoka bila kujijua....alishawahi kujikuta asubuhi ameamkia bafuni, sitting room, nje barazani, na sehemu nyengine wakati usiku alilala chumbani kwake, hali hii anayo kwa mda sasa na inamtokea karibu kila siku. Mpaka ameniambia mimi alitaka nimsaidie afanye nini kuepukana na hali hiyo? Na mimi nalifikisha humu jf wenye uelewa tumsaidie huyu dada
 
Pole.
Fanya maombi kwa Jina la Yesu Kristo nawe utashinda. Usiogope Majaribu hayana budi kutokea, Lakini ole wake yule atayeleta Majaribu.
 
hizo ni ndoto tu na wapo wengi wa namna hyo. Sijui afanyeje ili kuepukana nayo.
 
Pole mkuu, huyo rafiki wako wa karibu anasumbuliwa na tatizo la sleepwalking au kwa kitaalam wanaita somnambulism au noctambulism. Hali hii inatokea zaidi utotoni na inafuata koo fulani fulani. Chanzo chake hakifahamiki lakini inafikirwa kuwa inatokana na kutokokomaa kwa ubongo. Matibabu yake ni kutumia dawa zinazopoza ubongo katika dozi za chini. Ukimpeleka kwa daktari wa vichaa atapata ufumbuzi uliotengemaa.
 
mapepo yanamsumbua dadayetu huyo ajifunze kumtegemea yesu wala hata ona huo ujinga.mimi kwa miaka9 kila nikilala majinamiz yananigandamiza kila siku after deliverence nakumtegemea yesu nakusar bfore sleeping imebak story.mpe pole yataisha
 
Hakuna jina liwezalo kulishinda jina la yesu, mpe maisha yako serios utashangaa
 
Habari wana jf, poleni kwa kazi kubwa ya ujezi wa taifa, nina rafiki yangu wakaribu sana (mwanamke) anatatizo la kuota ndoto mbaya, anaweza kuota kama sauti inamwita kwa jina lake nje tena hua anatoka bila kujijua....alishawahi kujikuta asubuhi ameamkia bafuni, sitting room, nje barazani, na sehemu nyengine wakati usiku alilala chumbani kwake, hali hii anayo kwa mda sasa na inamtokea karibu kila siku. Mpaka ameniambia mimi alitaka nimsaidie afanye nini kuepukana na hali hiyo? Na mimi nalifikisha humu jf wenye uelewa tumsaidie huyu dada
Huyo Mwanamke atakuwa na shetani Dume ndilo linalo msumbuwa Mwambie aweke chini ya mto wake wa kulalia Tangawizi kavu punje moja hatoota tena ndoto mbaya iwe hiyo Tangawizi kavu Chini ya Mto kila siku asiitowe tena atumie kisha uje hapa unipe Feedback.
 
Maombi? Hapana

Maombi hapana ??? Sasa unataka msaada gani kama wewe mwenyewe huitaji maombi na uamini katika maombi? Wewe endelea kupuuzia maombi kuna siku ndoto hizo zitahamia kwako utajikuta utajikuta umeamkia pabaya ! omba bwana, maombi hayaongopi.
 
Huyo Mwanamke atakuwa na shetani Dume ndilo linalo msumbuwa Mwambie aweke chini ya mto wake wa kulalia Tangawizi kavu punje moja hatoota tena ndoto mbaya iwe hiyo Tangawizi kavu Chini ya Mto kila siku asiitowe tena atumie kisha uje hapa unipe Feedback.

Asante mkuu nitakuletea majibu
 
Huyo Mwanamke atakuwa na shetani Dume ndilo linalo msumbuwa Mwambie aweke chini ya mto wake wa kulalia Tangawizi kavu punje moja hatoota tena ndoto mbaya iwe hiyo Tangawizi kavu Chini ya Mto kila siku asiitowe tena atumie kisha uje hapa unipe Feedback.

Mkuu leo nimepata majibu ya tangawizi; ameniambia bado hajaona mabadiliko yeyote na amefanya kama nilivyomuelekeza
 
Back
Top Bottom