SoC01 Ni jukumu letu sote kuhakikisha Kuna amani nchini kwetu

SoC01 Ni jukumu letu sote kuhakikisha Kuna amani nchini kwetu

Stories of Change - 2021 Competition

Almachius Elizeus

New Member
Joined
Sep 19, 2021
Posts
1
Reaction score
1
Kabla ya yote ninataka ujifikirie kama mwimbaji anayependa kucheza, ukifanya mazoezi katika chumba chako cha kulala maneno mapya ambayo yalikutokea jana usiku…

AU kama mjasiriamali anayefanya mipango ya kuanza biashara mpya ambayo wewe na marafiki zako 4 mmeamua kuianza. baada ya mawazo mengi, majadiliano na utafiti..

AU kama mkulima ukilisha ng'ombe wako / ngamia na mbuzi jioni wakati wa kurudi kutoka mashambani kwako…
AU kama mwanasayansi ameketi katika maabara yako akijaribu kufanya utafiti juu ya uharibifu wa mifumo ya ikolojia kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa, uchafuzi wa mazingira.

Ghafla unasikia kelele kubwa nje, ya kusumbua: sauti kubwa, maneno ya matusi,… inasikika kama mgongano mbaya kati ya vikundi viwili,… vilio mabomu na mitikisiko mikali, kama mkulima, Kama mjasiliamali, Kama mwanasayansi hofu itakutanda na hapo hutoweza kuendelea na kazi zako......(AMANI HAIPO TENA)😰

🤔Fikiria hii hali kwa dakika 2. Jibu umelipata? 👉Haya twende kasi
Kwasababu leo amani inaweza kutajwa kutoka kwa muktadha wowote iwe ugaidi, ghasia za jamii, amani ya mtandao n.k.
TUNAHITAJI AMANI.
Tunahitaji amani NCHINI kwa sababu ni nyumba yetu!

👉 Siku hizi, watu wamezuia matumizi ya neno 'nyumba' kwa jengo, linalindwa na kuta nne. Lakini tunahitaji kuelewa kuwa Nchi hii yote ni nyumba yetu. Wazee wetu waliishi katika misitu wakipambana na wanyama wakali lakini ona sisi tumebarikiwa kuwa na makazi mazuri nyumba nzuri za kuishi, kumbi za starehe, nyumba za ibada n.k lakini sisi wenyewe tunataka kujiaharibia Baraka hizi kwa kukosa AMANI.

👉Tunahitaji amani NCHINI ili askari wenye ujasiri, jinsi wanajitolea maisha yao kwa ajili yetu, hawahitaji kuifanya kazi hiyo bali wanaweza kuishi maisha ya furaha na familia zao, kama wengi wetu hufanya endapo Kuna amani NCHINI mwetu.

👉 Tunahitaji amani NCHINI ili pesa nyingi, ambazo zinatumika katika misheni ya kutunza amani na jeshi zinaweza kuokolewa na kutumiwa kwa faida nzuri. Kuna shida nyingi kama umasikini, ukosefu wa ajira, ukosefu wa fedha kwa miradi anuwai, ambayo inaweza kushinda kwa kupeleka pesa hizo kwa malengo haya.

🤝Sasa, hata ikiwa sababu hizi hazikuvutii, basi unaweza kufikiria juu ya amani kwa hitaji lako la kibinafsi. Vita na hali ya vurugu nchini hutuathiri, sio tu kisaikolojia lakini pia katika mambo mengine mengi. Vita vinaathiri biashara ya nchi, ambayo pia huathiri maisha ya raia. Kwa hivyo, ikiwa nchi yako ina vita, basi pia maisha yako yataathiriwa.

✍️AMANI NI UFUNGUO WA MAISHA.
Watu wengi utaja mahitaji muhimu ya binadamu Kama nguo, chakula na makazi. Ni kweli kabisa haya mahitaji ni muhimu lakini bila AMANI yote ni kazi bure.

👉CHAKULA. Kama nchi haina AMANI chakula pia hakiwezi kupatikana vyakula vitachomwa Moto madukani, magahala yatavunjwa mashamba yatachomwa Moto na kibaya zaidi watu watakufa kwa njaa, hii yote itakuwa sababu ya kukosekana kwa amani.

👉MAVAZI. Hakuna amani hakuna MAVAZI. Shuhudia nchi nyingi amabazo amani imepotea watu wao wanatembea miguu peku katika sehemu hatarishi za masalia ya moto ya Vita Kali ya wao kwa wao.

👉MAKAZI. Amani ikishapotea makazi yote usambalatika, nyumba zetu uchomwa moto mashule yetu uchomwa moto na kubomolewa na nyumba zetu za ibada zitabomolewa na kuchomwa Moto. Mpaka Sasa kila mtu anafahamu kuwa amani ndio imebeba maisha yetu ya kila siku. Ndio maana nadiliki kusema AMANI NI UFUNGUO WA MAISHA✍️.
Ni jukumu letu sote kuhakikisha Kuna amani nchini kwetu, maana tukiwa na amani Mimi nitaweza kwenda kazi, wewe utaweza kusafiri kutoka kwenu kijijini kwenda kwa mjomba mjini, shangazi nae ataweza kwenda kazini, baba na mama wateweza kwenda shamba kututaftia chakula.

Lakini ndugu zangu bila AMANI haya yote hayawezekani.
Tuache kushawishi ujinga, tuache kuvunja Sheria makusudi, tuheshimu viongozi wetu wa nchi hizo ndizo nguzo kuu za kuleta amani nchini kwetu.

👉Yataongelewa mengi ya muhimu amabayo unaweza kuhisi Ni muhimu kuliko hili ninalolisemea la AMANI lakini amini na kwambia bila AMANI hakuna kitachowezekana, utaambiwa fungua duka, anzisha kilimo cha matunda kinalipa, anza ufugaji wa samaki, unda kukundi cha vikoba n.k lakini yote hayawezekani Kama hakuna AMANI nchini.

👉Wahitimu tunaomaliza vyuoni tuwe mfano bora wa kueneza amani nchini kwasababu sisi ndio kundi kubwa tunaotambukika Kama wasomi wenye uelewa wa juu. Tuonyesheni uelewa wenu na taaluma zenu kwa kuwataka wananchi kuilinda amani ya nchi.

👉Amani ni neno lenye nguvu sana na lenye ufanisi. Ni nini kinachotufanya tuhisi kuwa maisha yetu ni ya amani au ni laini na rahisi?

👉Thamani ya amani katika maisha ya mtu ni kitu ambacho watu wengi huchukulia kawaida. Unapaswa kumwuliza mtu ambaye hakulala kwa sababu ya kelele isiyotarajiwa, ni nini mtu huyo angependa, na jibu ni amani na utulivu.

👉Pia, ikiwa unaishi katika msukosuko wa hisia, maamuzi yasiyofaa, watu wabaya, shida nyingi, unapaswa kuthamini amani, unaweza kufikiria wazi, na hii ndiyo sharti la msingi la kupata matokeo bora katika kila eneo la maisha yako.

👉Kuhoji, kuuliza na kukosoana vyote vinawezekana kwa kuthamini amani na kuitumia amani. Haina sababu ya kuoji kwa hasira, kuuliza kwa kufoka, matusi na misutano, hizo ndizo sababu kubwa za mizizi ya uvunjifu wa amani, tuziepuke.

👉Tuipende nchi yetu, viongozi wetu, wakubwa zetu, wadogo zetu na wazee wetu maana Amani ndio muongozo mkuu wa MAENDELEO YA NCHI✍️ yote unayopanga kuyafanya Kama hakuna kipengele kinachohusu amani kamwe huwezi kufanikiwa.

MWISHO. Ili tufanikiwe tunatakiwa kufuata vitu vitatu muhimu. 1 AMANI 2. AMANI 3.AMANI.✍️
 
Upvote 1
Back
Top Bottom