ramadhani kimweri
Senior Member
- Apr 22, 2016
- 181
- 179
Ukizaa mwana mwari, yani mtoto wa kike,
Wazazi muwe tayari, kuzichunga haki zake,
Dunia haiko shwari, Kuulinda utu wake,
Ni juu yenu wazazi, Kumfunza kwa makini,
Nyakati hazifanani, hilo mlijue wazi,
nyuma miaka sabini, hakuna utandawazi
Hivyo kuweni makini, badilisheni malezi,
Leo kila kitu wazi, vimemwangwa hadharani..
Mitaa tunayo ishi, yenyewe ni changamoto.
Mazingira hatarishi, tunalelea watoto,
Ukiudharau moshi, utakuunguza moto,
Si salama zama hizi, sote tupo hatarini..
Nia na dhumuni hasa, niseme na wewe baba,
Usome hili darasa, chukua weka akiba,
Dunia ina anasa, imajaa mangaliba,
Jifunze ewe mzazi, mwenye watoto nyumbani
kiwa na bint ndani, ishi naye kwa makini,
Tena kaa naye chini, mwelezee kwa undani,
mweleweshe abaini, thamani yake ni nini,
Yote yenye utatizi, ayaweke akilini.
Dunia imechafuka, kumekosekana utu,
na imejaa vibaka, roho zao mbwa mwitu,
Kitu wanacho kitaka, kuharibu wana wetu,
Kuwa makini mzazi, chunga wanao nyumbani,
Vishawishi vya mapenzi, vimejaa kila kona,
muwekee vizuizi, tena mwambie kwa kina,
Matendo ya kipuuzi, yale yasio na mana,
Akatae waziwazi, wayafanyayo wahuni..
Hapa nashusha kalamu, beti nane nahitimu
masomo haya muhimu, ninatoa kwa awamu,
Na mjifunze nidhamu, na pia kujiheshimu,
Kulea nako ni kazi, tusifanyie utani.
[emoji2400]IBN KIMWERI( Baba juma).
ramadhanikimweri7@gmail.com
Moshi - Kilimanjaro.
TANZANIA.