Ni kitu cha ajabu sana hiki...watanzania kuanza kuwa na nyuso hizi za matumaini wakati mifukoni mwao bado hawana kitu ni jambo la ajabu saana!!Kama Mungu yupo kweli basi anaipenda sana Tanzania kuliko watu wanavyofikiri!! Na Watanzania kama hatutajifunza kwenye hili hata Malaika watakasirika na ghadhabu tutaiona
Una maana ipi kaka? Wewe si mmoja wa watanzania ambao wanaoangalia mwangaza kwa mbaali? Unaona namna akina Sabaya walivyojigeuza wao kuwa mapolice, wao mahakama na wao hao hao kutoa hukumu?Mi kitu nilichojifunza ni "heri kumfadhili mbuzi,utakunywa hata mchuzi..lakini si kumfadhili binadamu,binadamu si mtu mzuri" hili nimejifunza,na nitaitumia ktk maisha yangu kama kanuni,kuanzia juzi simuamini binadamu yoyote aisee
Pia jifunze kusema ukweli muda wote katika maisha yako!Mi kitu nilichojifunza ni "heri kumfadhili mbuzi,utakunywa hata mchuzi..lakini si kumfadhili binadamu,binadamu si mtu mzuri" hili nimejifunza,na nitaitumia ktk maisha yangu kama kanuni,kuanzia juzi simuamini binadamu yoyote aisee
Wanaogopa tu kuandamana ila wana furaha ya ajabu.....ni kweli kabisa!!Kwa kweli tumepata uhuru. Hata kwenye makundi ya WhatsApp unaona waliokuwa wanaogopa kabisa kuchangia chochote kwenye mijadala, sasa wanafunguka.
Mpaka wabunge pale mjengoni nao wamepata uhuru.....tukianza na Mh 'Supika'.
JPM alituweza kweli!
Adi spika kasema jamani semeni ukweli ili msaidie serikali kufanya mipango yake kwa ufanisi Msiogope msiogope!!Kwa kweli tumepata uhuru. Hata kwenye makundi ya WhatsApp unaona waliokuwa wanaogopa kabisa kuchangia chochote kwenye mijadala, sasa wanafunguka.
Mpaka wabunge pale mjengoni nao wamepata uhuru.....tukianza na Mh 'Supika'.
JPM alituweza kweli!
Baba huu ni kama uhuru mwaka 1961wa Tz wamefurahi sijapata kuona hizi siku, nikama tumepata uhuru tena duh
Kaka hata kuongea kuhusu mwenendo wa nchi yako ilikuwa shidah, huyu mjinga mjinga Msiba ni wa kuwatukana kina Kikwete na kinana kweli? Hapo ndipo mwendazake alipokuwa katufikisha.Anayebisha basi hayuko sawa..jamani tulitishwa mnooo khaaa
Nimefanya uchunguzi wangu binafsi nimeona na kujiridhisha pasi na shaka kwamba nyuso za watanzania zimefunguka!! Kuna ki faraja fulani ndani yao. Vijiwe vingi sasa vinaanza kuongea mambo ya matumaini...
Ni kama nchi imepata uhuru vile !! Kuna kitu kwa kweli kimo ndani ya hawa watanzania.
Nafikiri hata na nyie wenzangu mmeona wenyewe hali ya nchi ilivyo kwa hizi siku tatu nne....
Watalaam wa saikologia ya binadamu pia wataniunga mkono....