johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Nilipowaona viongozi wa Chadema wakitoka Segerea na vipara ndio nikajiuliza, ukikubali kulipa faini haupewi walau muda kidogo wa kukamilisha taratibu za kiuhasibu?
Kwa maana kitendo cha kunyolewa nywele na kutupws gerezani ni kwamba tayari una namba inayoonyesha umeingia lini na utatoka lini labda upite msamaha wa Rais hapo katikati ndio utawahi kutoka.
Hii sheria ipitiwe upya mfungwa akikubali kulipa faini apewe muda fulani labda siku 3 na akishindwa ndio atupwe gerezani na hasa faini yenyewe inapohusisha kiasi kikubwa cha fedha.
Kuna nchi hapa Duniani hata kifungo cha jela hakianzi siku hiyo hiyo unapewa wiki mbili za kuweka sawa mambo ya familia yako ndio unaripoti gerezani.
Maendeleo hayana vyama!