Ni kawaida lakini si kawaida

Ni kawaida lakini si kawaida

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Katika Dunia ya Sasa au tuseme Dunia ilipofikia kuna mambo kabisa unayaona si ya kawaida lakini yamegeuzwa kuwa ya kawaida sana.

Kawaida lakini si kawaida.
Siku zote ilikuwa ni ajabu sana kijana mdogo kuwa katika mahusiano na mbaba/mama mtu mzima umri sawa na mama yake.

Ilikuwa ngumu sana na hata ikitokea basi kama sio kutengwa na jamii ni kupigwa viboko hadharani.

Cha ajabu sasahivi mambo yamebadilika, leo hii wanaitwa Mishangazi/mbaba.

Majina yalianza kubadilishwa mara sugar mamy/Serengeti nk. Kwa sasa kumiliki lishangazi imekuwa ni kawaida na si kawaida tu bali ni ujanja. Binti kutoka na mwanaume sawa na Babu /baba yake imekuwa kawaida sana.

Kuvunja Ndoa zamani ilikuwa si kawaida kabisa but Kwa Sasa ni kawaida tu kijana wa umri miaka 24 unamkuta kaachana na wanaume/wanawake 3 ni kawaida tu.

Imekuwa kawaida sana mabinti kuzalia nyumba lakini hapo nyuma haikuwa kawaida kabisa!

Hapa tunapo wasema singo Maza inaonekana tuna wanyanyapaa lakini ukweli ni kwamba imekuwa kawaida kabisa kuzalia nyumbani na bila kukemea Kwa nguvu zote Hali itakuwa mbaya mno!!

Haikuwa kawaida binti uzae kwenu bila KUOLEWA ilikuwa ngumu mnoo.

Wanawake walio olewa kutambiana michepko walio nayo Nje ya ndoa zao.

Huwezi amini kwenye ndoa zetu wanawake wana tambiana kuwa na michepko imekuwa KAWAIDA SANA. Sema huwezi ambiwa tu lakin kwa majasusi watakubaliana namimi kuwa hii nayo imekuwa life style kwenye ndoa nyingi.

Mambo ni mengi sana ni kawaida kumbe si kawaida.
Mwanaume kusuka nywele
Kuweka Pini/ hereni
Kuchora tattoo
Na mengine mengi.
Je! Ni kawaida Gani kwako ambayo Kwa jamii Yako unaona si kawaida kabisa?

FB_IMG_1709042248840.jpg
Karibu
 
Back
Top Bottom