Ni kawaida Mambo haya kutokea kwenye "MISIBA"' au Kwenye "Harusi"

Ni kawaida Mambo haya kutokea kwenye "MISIBA"' au Kwenye "Harusi"

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
1616175294358.png


NI KAWAIDA HAYA KUTOKEA KWENYE "MSIBA" AU KWENYE "HARUSI"

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Harusi na msiba ni matukio muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Tofauti ya matukio haya mawili ni kuwa tukio moja kila mwanadamu hutamani kulifanya lakini wachache ndio hubahatika kufanya. Tukio hilo ni harusi. Wakati Tukio la pili hakuna mwanadamua anayetamani kulipitia au litokee lakini kwa bahati mbaya tukio hilo kila mwanadamu lazima alipitia.. Tukio hilo ni Msiba au Kifo.

Sio kila mmoja atafunga HARUSI lakini kila mmoja wetu lazima atakufa, hilo hakuna ubishi. Harusi inahitaji kujipanga, lakini kifo hakina kujipanga, yaani kifo ujipange usijipange kufa lazima utakufa,

Kwenye Harusi watu hutoa machozi ya furaha huku wakicheka lakini kwenye Msiba watu hutoa machozi ya huzuni wakilia.

Harusi inahitaji mualiko lakini msiba haunaga mualiko na sababu kuu ni kuwa, kimoja wapo huwatokea binadamu wote wakati kingine ni kwa binadamu wachache.

Harusi na Msiba vinafanana kwa sehemu kubwa wakati huo huo vinatofautiana kwa sehemu kubwa. Wakati Harusi ikihusu Muungano wa watu wawili, Msiba humaanisha utengano.

Harusi ina MAHARUSI, Bwana na Bibi
Msiba una Marehemu, mimi au wewe au yule(Yeyote)

Sio ajabu watu wasiifurahie Harusi yako, na nimeshashuhudia mara kadhaa watu wakijisikia vibaya pale wasikiapo fulani anafanya harusi na fulani, badala ya kufurahi. Hii ni dunia wala usistaajabie jambo hio.

Hujawahi kusikia watu wakiponda Maharusi, si ajabu ukasikia Bwana harusi ni kafupi kama nyundo, au Bibi Harusi hata hajapendeza.. Kama haitoshi vishankupe husonya na kuteta hata hawajaendana. Hata hivyo ni kawaida kusikia kashfa ya chakula kibaya katika maharusi. Hii ni kawaida.

Sio ajabu vikao vya kamati ya roho mbaya kukaa hata usiku wa manane kupanga njama ili harusi isifanyike na maharusi watarajiwa wagombane ili harusi ife kifo cha mende. Na kama harusi ikifanyika bado kamati haitasaimu amri itaendeleza figisu figisu chini kwa chini mpak ndoa ivunjike. Kisha yakitimia; ndoa ikivunjika, ile ile kamati ya roho mbaya italipuka kwa shangwe wakishangilia kutengana kwenu.

Kwenye misiba sio kila mtu huomboleza au kuhuzunika, hasha! wapo watu hufurahia misiba ya watu wengine, wengine huweka sherehe kabisa na kula na kucheza kama sio kulewa. Ni jambo la kawaida mambo haya wala sio jambo la ajabu.

Sio kosa mtu kufurahia msiba wa mtu mwingine ilimradi anasababu ya msingi.

Ninakumbuka Farao allivyozama na jeshi lake bahari ya sham mbele ya macho ya Wana wa Israel, nani hakuusikia wimbo wa Miriam Dada yake na Nabii Musa aliouimba akishangilia kufa kwa farao na jeshi lake, sio yeye tuu hata waisrael wote walishangilia, Musa akiwemo.

Fahamu kabisa, siku ukifa wapo watakaoomboleza na wapo watakao sheherekea na kuweka sikukuu, kabisa. Hiyo ni kawaida wala usije ukashangaa.

Fahamu kabisa siku ukioa, wapo watakanuna, kuhuzunika, na kuchukia. Hayo ndio maisha.

Hata hivyo lazima tuseme kitu;

Sio jambo dogo kufurahia Msiba wa mtu mwingine, lazima iwapo sababu kubwa sana ya mtu kufurahia msiba wa mtu mwingine. Hata hivyo sio kosa wala sio dhambi.

Moja ya mambo ambayo hufanya watu wafurahia vifo vya wengine, ni kutokana na tabia za baadhi ya marehemu, mathalani uonevu, dhuluma za mali, mauaji, wizi na mambo mabaya mengine. Ndio maana hata Goliath alipouawa na Daudi Wayahudi walishangilia na kufanya sherehe, hii ni kutokana na sababu kuwa Goliath chini ya utawala wa wafilisti alikuwa mwiba kwa waisrael.

Mbali na misiba, watu kuchukia na kujisikia vibaya unapofanya harusi sio jambo dogo asilani ijapokuwa linawezekana kwani linatokea kila siku. Mathalani huwezi kuniambia umchukue mchumba wa mtu alafu uende ukafanye naye harusi alafu utegemee uliyemchukulia mchumba atakusapoti kwenye harusi yako. Sio kweli.

Nakubali na siwezi kujisahaulisha kuwa; wapo watu wenye roho mbaya ambao wanachuki zao tuu za asili, hata hukuwakosea, hukutenda baya lolote lakini bado hawatataka ufanikiwe, ufurahie maisha, au ufanye maendeleo ikiwemo kufanya harusi nzuri na kuishi na mkeo/mumeo kwa amani. Lakini watu hawa kikawaida ni wachache mno sana. Kwenye kumi basi mmoja.

Pia wapo wenye roho mbaya na chuki zisizo na sababu ambao siku ukifa watashangilia utadhani uliwahi kufanya makosa makubwa ya kuua mtu. Zingatia pia, watu hawa ni wachache, hivyo ukiona wapo wengi wanaofurahia anguko lako ujue kuna sehemu haukufanya vyema.

Kwenye maisha ya binadamu lazima tujitahidi kutenda wema kwa kadiri tuwezavyo, wema ndio sifa na nguzo kuu ya kujivunia. Usijivunie elimu, cheo, mamlaka, uzuri au utajiri hautakusaidia chochote.

Watendee watu wema bila kuwabagua ili nao siku ukifa wakupe heshima bila kukubagua, sio wengine wanakusifu alafu muda huo huo wengine wanakuponda kwa mambo mabaya ya kweli uliyoyafanya.

Mimi sioni ajabu kwa Marehemu kupondwa au Maharusi kupondwa ikiwa ndio ukweli. Mimi mwenye nilishasemaga, siku nikifa msinionee haya, nichaneni makavu, sio muniletee unafiki wenu kwenye msiba wangu. Kama huwezi kusema mabaya na mema yangu kaa kimya siku hiyo. Sitaki mambo ya unafiki wa mila potofu za kizamani hapa.

Maharusi wapondeni ikiwa kunasehemu ya kuponda, yaani uibe mchumba wa mtu watu wakusifie, watakusifia ndugu zako, pumbavu!

Mwisho, tuishi kwa kupendana, na upendo ndio huo kuishi billa kubaguana, kuoneana, kudhulumiana, kuumizana.

Ulikuwa nami mwana wa Tibeli, Nyota ipaayo yenye mbawa mbili.

Robert Heriel
Taikon wa fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ata alivyokua hai tuliposema tupendane yeye alisema piga kazi
 
Ata alivyokua hai tuliposema tupendane yeye alisema piga kazi

Ulikuwa mtazamo wake, nafikiri aliwahi kusema pia watanzania wapendane.

Ila kusema sio kutenda, watu kama Taikon hufuata matendo sio maneno
 
Me nauliza tu jamani network imezma kwngu tu au nyote mana JF tu ndio ina network kuanzia hivi usiku[emoji27]
 
Back
Top Bottom