Sababu ni nyingi.Siku hizi ndoa nyingi ni ya kulazimishana. Kwa mfano wanaume wengi siku hizi wanalazimika kuoa bila kupanga kufanya hivyo. Unakuta mwanaume ana uhusiano wa kimapenzi na msichana huku akiwa hana mpango wa kumwoa lakini kumbe msichana anakuwa ameshapanga kumtega. Kwa hiyo mwanaume wa namna hiyo akimwoa msichana huyo hatakuwa na mapenzi ya kweli. Pia wanawake wengi wakiingia katika ndoa wanashindwa kuonesha mapenzi ya dhati kwa waume zao. Wanakuwa wananuna mara kwa mara. Kwa hiyo mwanaume anaanza kutafuta nyumba ndogo.Pia kuna suala la kuridhishana katika tendo la ndoa. Wanaume wengi hushindwa kuwaridhisha wake zao katika tendo la ndoa. Kwa hiyo wanawake hulazimika kuwa na wanaume wa nnje.Kwa upande wa wanawake wapo wengine wanapofanya tendo la kujamiiana na waume zao wanalala tu bila kushughulika.