Ni kiasi gani cha Kodi ulipiwa ukiingiza Body ya gari bila Chasis toka nje ya nchi???

Muhamala

Senior Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
101
Reaction score
88
Kwema wakuu.

Bila shaka mnamalizia wikiendi kwa utulivu kabisa.

Niende kwenye swali langu moja kwa moja kuwa hivi ninapo nunua/agiza body la gari bila chasis kutoka nje ya nchi kuja hapa nchini kwetu ni njia gani ya makadilio ya kodi hutumika ili kupata kiasi cha kodi kinachopaswa kulipiwa pindi body la gari linapokuwa limefika??? Naombeni msaada katika hili wakuu najua humu wapo waliowahi kuagiza body ya gari toka nje ya nchi.

Karibuni kwa michango yenu wakuu.
 
Mkuu hakuna utaratibu unaoeleweka, labda lipeleke uganda utalipia kama screpa then peleka gari yako uganda kavalishe bodi urudi.
Bonge la akili mkuu ila shida sasa hapo gharama inaongezeka.
 
Mkuu hakuna utaratibu unaoeleweka, labda lipeleke uganda utalipia kama screpa then peleka gari yako uganda kavalishe bodi urudi.
Uganda wao huchaji kama screpa mkuu??
 
Hii issue iliwasumbua sana Befoward mpaka wakaacha kuleta nose cut na baadaye kufunga kabisa warehosue yao ya spare pale Tabata. Hakuna mfumo maaalum it seems wa kucharge vipande vipande vya gari vinavyoingizwa nchini...
 
kuna kipindi darexpress waliagiza bodi za marcopolo hawakurudia tena sijui kiliwakuta nini!
Duuuh hapo majibu tushayapata kuwa walipigwa kodi ya kufa mtu. Sasa kwa mtindo huu watakosa mapato kwa watu wanaoogopa kuagiza wakihofia tozo kubwa la kodi
 
Ndiyo mkuu norsecut Uganda wanauza kama screpa sie unaambiwa ni gari
Ningekuwa naishi Bukoba ningefanya kama ulivyoshauri mkuu ila duuh kutoka Dar to Uganda ni kipande haswa.
 
Hii issue iliwasumbua sana Befoward mpaka wakaacha kuleta nose cut na baadaye kufunga kabisa warehosue yao ya spare pale Tabata. Hakuna mfumo maaalum it seems wa kucharge vipande vipande vya gari vinavyoingizwa nchini...
Hivi kumbe BeForward walifunga warehouse yao pale. Sasa hii serikali yetu nayo vipi mbona inalala sana.
 
Ndiyo mkuu norsecut Uganda wanauza kama screpa sie unaambiwa ni gari
Nchi yetu kweli ni shida sasa tumeshindwa nini kuwa na sheria kama ya Uganda jirani yetu huyo.
 
Kila mtu atafikiwa kisha wimbo tutaimba mmoja tu!!! Muda ni mwalimu mzuri sana
 
Kila mtu atafikiwa kisha wimbo tutaimba mmoja tu!!! Muda ni mwalimu mzuri sana
Fafanua vizuri mkuu wengine tumeishia darasa la 7D kwahiyo vichwa vyetu ni vigumu sana kunyambua mafumbo magumu kama lako 🙂🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…