Ni kiongozi gani hubeba maono ya mkoa au jiji - ni RC, RAS au Mkurugenzi?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Napata Wakati mgumu kujua kimfumo ni Kiongozi yupi anayebeba maono au vision nzima ya mkoa au jiji? Najiuliza kwa sababu juzi wameteuliwa wakuu wa Mikoa na niliamini wao ndio wasimamizi wa malengo, maono na mipango ya Mkoa. Kinyume chake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma pekee ndiye aliyetoa hotuba inayoweza kuonekana kama ana vision flani dhidi ya Mkoa wa Dodoma. Waliobaki hauoni kama wanajua wanataka kufanya nini na Kama awajui, usipotoa vision yako kwenye hotuba zako za awali itakuwa ngumu kutoa vision yako huko mbele uendako.

Mfano mzuri, Rais anapoapishwa uenda bungeni kwa mfumo wa kwetu nakueleza ana maono gani. Si maono yote yapo kwenye ilani Bali maono mengine utokana na utashi wake na kiu aliyonayo ikiunganishwa na uwezo binafsi aliojaliwa na Mwenyenz Mungu.

Niombe tujiulize nakumkumbusha huyo mwenye vision ya eneo flan kwamba waliochini yake wanataka kujua anapotaka waelekee ili wamfuate. Sidhani Kama kwa Mfano anachotamka kwenye mikutano na watendaji na hotuba za RC Mwanza ndio vision ya Mwanza. Sidhani Kama alichozungumza RC Dsm ndiyo hotuba ya vision yake dhidi ya DSM nk.

Tungetamani kujua tunakwenda wapi? Au Kama RC na DCs siyo Marais wa Mikoa na wilaya Basi Marais wajitokeze watuambie cc waongozwa vision ni nini?
 
Mkurugenzi ndio kila kitu, mipango yote ya muda mfupi na mrefu anayo mkurugenzi.

Wengine wapo kutatua matatizo, changamoto na kero za wananchi zinazojitokeza kwenye jamii.

Pia kusimamia utekelezaji wa Ilani ya chama tawala.
 
Wanasimamia mipango ya serikali ambayo tayari ipo na inaendelea kutengenezwa......watendaji ndo wenye vision, siyo wanasiasa.
 
Kwani kuna mkurugenzi wa mkoa?
Kazi zake ni nini?
 
Wakurugenzi wa Halmashauri ndio wenye kila kitu. Hao ma rc na dc hamna chochote zaidi ya ulinzi na usalama na siasa. Na kuwasumbua hao wakurugenzi.
 
Napata Wakati mgumu kujua kimfumo ni Kiongozi yupi anayebeba maono au vision nzima ya mkoa au jiji? Najiuliza kwa sababu juzi wameteuliwa wakuu wa Mikoa na niliamini wao ndio wasimamizi wa malengo, maono na mipango ya Mkoa. Kinyume chake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma pekee ndiye aliyetoa hotuba inayoweza kuonekana kama ana vision flani dhidi ya Mkoa wa Dodoma. Waliobaki hauoni kama wanajua wanataka kufanya nini na Kama awajui, usipotoa vision yako kwenye hotuba zako za awali itakuwa ngumu kutoa vision yako huko mbele uendako.

Mfano mzuri, Rais anapoapishwa uenda bungeni kwa mfumo wa kwetu nakueleza ana maono gani. Si maono yote yapo kwenye ilani Bali maono mengine utokana na utashi wake na kiu aliyonayo ikiunganishwa na uwezo binafsi aliojaliwa na Mwenyenz Mungu.

Niombe tujiulize nakumkumbusha huyo mwenye vision ya eneo flan kwamba waliochini yake wanataka kujua anapotaka waelekee ili wamfuate. Sidhani Kama kwa Mfano anachotamka kwenye mikutano na watendaji na hotuba za RC Mwanza ndio vision ya Mwanza. Sidhani Kama alichozungumza RC Dsm ndiyo hotuba ya vision yake dhidi ya DSM nk.

Tungetamani kujua tunakwenda wapi? Au Kama RC na DCs siyo Marais wa Mikoa na wilaya Basi Marais wajitokeze watuambie cc waongozwa vision ni nini?
RAS ndiyo mtendaji mkuu wa mkoa hivyo anabeba maono yote maana RC zaidi ya vikao hana kazi ya maana
 
Kwani kuna mkurugenzi wa mkoa?
Kazi zake ni nini?

Mkoa hauna Mkurugenzi una RAS huyu ni sawa na Katibu Mkuu Wizarani

Waziri= RC

Katibu Mkuu=RAS
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Sawa. Kwa hivyo, ki madaraka nikisema wakurugenzi wa halmashauri zote ndani ya mkoa wapo chini ya RAS na hivyo chini ya mkuu wa mkoa nitakuwa sahihi?
 
Watumishi wote wa Serikalini wapo Chini ya RAS! RAS anareport kwa Waziri wa TAMISEMI moja kwa moja! Hapo ndiyo huwa sielewi,nafasi ya “U boss” wa RC kwa RAS unatokea angle ipi? Pengine kujibu hili swali tujiulize kwanza Katibu Mkuu wa Wizara yupo chini ya Waziri? If Yes basi na kwa RAS itakuwa hivyo hivyo.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom