Ni 'Kitchen Party' au 'Bedroom Party'?

Hivi kwa maisha ya leo unategemea eti wakati wa maandalizi ya harusi ndiyo wa kumfundisha binti habari za kitandani?? Nafikiri kwa vijana wa siku hizi wanaharibu kitanda cha ndoa kabla ya ndoa yenyewe!!! Na kwa mantiki hii huwa wanakuwa wameshafahamiana vya kutosha kwa masuala hayo ya kitandani zaidi kuliko hata tabia zao halisi??? Tuepukane na enzi zetu za ujima mtu ulikuwa huruhusiwi hata kumkaribisha mchumba nyumbani akiwa peke yake bila kusindikizwa na ndugu wa karibu na unaheshimu siku ile tukufu ya ndoa!!

Hebu jamii ibuni kitu kingine cha kuwaasa au fundisha hawa mabinti na vijana wa kiume hasa kuhusu kulinda ndoa zao maana zinavunjika mno baada ya siku chache/miezi/mwaka/miaka michache tu. Ni aibu kwao na familia zao. Mungu husika kwa malezi ya watoto wangu, wajukuu, vitukuu. vilembwe na vilembwekeze ili wadumu katika ndoa zao kama walivyodumu za mababu zetu na wazazi wao. Amen.
 
umesomeka mkuu!UKWELI MTUPU....!nimegonga kale kabatani😀
 
kweli lakini hizi kitchen party hazina maana kama ndo mambo haya... halafu girls wasikuhizi wanajua kilakitu sijui wanafundishwa nini...? wanawake wanakosa mambo ya maana ya kufanya ndo maana wanaanzisha hizi kitchen parties... where else will they gossip and talk dirty ... arghhhhhh

Lakini issue inarudi kwa wazazi au wanaume vipi wawaruhusu watoto wao (children) wasikilize mambo ya wakubwa... haifai kabisa...wakatazeni wake zenu na watoto wenu ku attend these kind of parties...
 
wanaenda kwa ajili ya vyombo
 
ooow my bad ... I never attend these kind of parties so I wouldnt know
ndivyo ilivyo!siku hizi zipo zile ambazo HAKUNA MICHANGO!,BITES ZINAKUWEPO,KINYWAJI UNAJILIPIA-SHARTI NI LAZIMA UJE NA VYOMBO
 
inategemea na maadili ya kabila lenyewe, makabila kama ya kwetu kaskazini ni wagumu sana kusema yale mambo ya ndani sana, huwa wanasema mambo ya juujuu kama usafi, kupika n.k lkn intention yao inakuwa ni zawadi za yule binti kwenda kuazia maisha. Watu wa Pwani naomba mnisamehe lkn kitchen party za watu wa pwani ni balaa, hawana aibu hata kidogo, huko ndo unakutana na mafiga matatu, kuna kusasambua, kuweka godoro binti anafundishwa kukatika kiuno na mambo kama hayo . alafu mbaya zaidi mkanda unakuwepo kwa kumbukumbu za baadae. hii kwa kweli inazidi kuvuruga maadili yetu maana hata waume zetu wanaziona.
Au kaka na wewe uliona mkanda wa mamaaaa?
 
Wa kwangu tulikubaliana asifanyiwe na hilo lilkuja baada ya yeye kunambaia alichokuwa anhitaji ni vyombo; baada ya harusi kulikuwa na mzungu anaondoka mie nikaongea naye na akaniuzia vyombo vyte vya ndani!

Kwa hiyo ushauri kwa maharusi wapya ni kuwa kuweni na maamuzi yenu juu ya nini mnakitaka sio kukurupuka kuiga kila kitu mtaishia kupata hasara kuliko faida!
 

sasa ndugu kama wanawake wanaona kama asilimia kubwa waipeleke vyumbani, wanaume mnataka nini tena?
 
Haya mambo ni ya akina mama haya, kwa mila za kwetu sitakiwi kuingilia mambo yao,
Isipokuwa nawauliza nyie wanaune wenzangu mnaoendaga kwenye kitcheni party mnaenda kufanya nini?halafu nawauliza akina mama, hao wapiga picha sijui nini utakuta yote midume inakuwaje? Mwisho naona wote hamridhiki na sherehe hii. Mnaonaje mkimpa masharti MC
kuwa tunataka hiki hatutaki hiki sherehe itanoga tu.
 

Laaziz hapo umesema ukweli kabisa! Halafu cha ajabu hao watoa mada wengi wao wameachika.

Unakuta mama ana mtoa mada ana watoto watatu kila mtoto na baba yake, kashaolewa na kuachika mara sita! Sasa atamfundisha nini kizuri binti anayeingia ndani ya ndoa? Jamii yetu inabidi ibadilike sasa jamani!
 

Kwa uhakika kitchen party ni imeshapoteza maana, ni kama ccm kwa nchi yetu!
 

Nyamayao sijawahi kusikia habari hizi za mafiga matatu ila naona hawa wamevuka mipaka hawana maadili ya ndoa zaidi wanataka kuvunja ndoa na kuleta magonjwa katika ndoa za watu..
Nadhani hao makungwi walikuwa mashangingi waliokubuhu na si ajabu hawana ndoa .....
kha imenisikitisha sana hii
 
Nini Kifanyike?
Hivi zamani bibi zetu walikuwa wanafanyiwa kparty?:confused2::shocked:
 

Nafikiri hawa wenzetu hawataki kusema moja kwa moja kuwa ni 'bed room party' ila 'kitchen' inasimama badala ya 'bed room' kwa maana ya kwamba jikoni kuna pilika pilika kama zile za chumbani - jikoni kuna kinu na mwichi na chumbani kuna kinu na mwich; jikoni kuna kukoroga na chumbani kuna hiyo shughuli, n.k. Hivyo kitchen ni maana ya pili au ni slang ya wanawake kuhusu shughuli za chumbani; yaani alivyo mzuri jikoni kumpikia mumewe basi vivyo hivyo afanye na chumani!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…