music mimi
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 485
- 876
Ebu shea na sisi pengine wale wanaorithi kila kitu toka kwa wazazi watakiepuka kwenye malezi ya watoto zao.
Mimi nilikuwa nakatazwa sana kucheza kwenye majumba ya majirani. Wazazi wangu muda wote walitaka wanione nyumbani tena nikiwa mtulivu. Niliamini kutembea kwenye nyumba za jirani ni vibaya.
Hii imenifanya nimekuwa sio mtu wa kujichanganya na muoga wa watu. Moja kati ya mitihani yangu mikubwa ni kuanzisha ushikaji na watu naokutana nao kwa mara ya kwanza. Naamini ni kwa sababu udogoni nilinyimwa skills za kucommunicate na wenzangu.
Kingine mimi nilipokuwa mdogo nilikuwa napenda sana kuchezea cherehani ya mama. Ñilikuwa napenda kushona nguo. Lakini bi mkubwa alikuwa ananiweka mbali na nilishachapwa mara nyingi sababu ya cherehani. Mwisho nikaacha.
Kuna wakati nikiwa mkubwa nilikuja kufanya connection ya mapenzi yangu kwa cherehani na fashion.
Napenda sana kuvaa nguo nzuri. Uhenda ningekomaa na cherehani ningekuwa designer mzuri wa mavazi. Of course nimesoma mpaka chuo kikuu na nna ajira lakini sina tena nguvu ya kusema niwe nna factory yangu kuzalisha maybe suti au magauni. Bado nna uoga uleee wa cherehani.
Ebu shea experience yako na wewe.