Chapakazi
JF-Expert Member
- Apr 19, 2009
- 2,874
- 316
Huu kama mwaka wa uchaguzi ningependa kupata maoni yako juu ya kitu kimoja ambacho ungependa serikali ya awamu ya tano ikipe kipaumbele. Jaribu kuwaza kama umepata nafasi ya kukaa na Wagombea Urais na kuwapa dokodoko zako. Ni kitu gani cha kwanza utawaomba wafanye? Na sio kwa jimbo lako, bali kwa manufaa ya Tanzania nzima. Au niigeuze kivingine, kama wewe unapewa nafasi ya kuwa rais wa awamu ya tano, je ni kitu gani KIMOJA ungependa kukumbukwa kwa kufanya? Ningependa kupata maoni yenu kwa kusudi la kujua muelekeo na matumaini yetu. Niwie radhi, maana hii inaangalia serikali in a very narrow perspective.
Mimi binafsi ningesema viwanda. Ningependa tuwe industrial powerhouse hapa East and Central Africa, hasa ukizingatia huu muungano na muelekeo wake. Hivyo ni muhimu awamu ya tano iweke msingi mzuri wa kuwezesha hili. Wewe je?