Ni kitu gani...?!


Nimekuelewa ila kusema kwamba yanayoonekana baadae yanakua tabia ambazo zilikuwepo tangu mwanzo napingana na wewe maana kwa kiasi kikubwa mapenzi yanapoanza kila mmoja hua anafocus kwenye kumfurahisha/kumridhisha mwenzake.Kama anatabia za kufoka foka wala hutojua...kama ni mvivu wala hutogundua...kama ni mgomvi ndo kabisa hatokuonyesha mpaka siku atakapochoka kuficha uhalisia wake ndo unashangaa ghafla ukirudi nyumbani jiko limenuna..kila unachofanya anagomba...akikasirika kidogo mkono hewani na matusi juu.Hamna mtu hata mmoja anaeweza kuanza mahusiano na uhalisia wa aina hiyo...hua yanakuja baadae mtu anapoona kwamba ameshakuweka mkononi/kitanzi cha ndoa na vitu kama hivyo.Ndo maana watu hawaishi kulalamika kuhusu makucha ya wenzi wao yanavyochomoza baada ya kuwekana kwenye himaya!

Pili...jiulize kama mtu alianza kwa kujionyesha kwamba hana hizo tabia ambazo zinachomoza baadae kwanini asiendelee kuzificha kama kweli anakuthamini/penda na hataka kukuumiza au kukukera?!Maana tayari unajua kwamba anaweza sana kuzuia hasira zake pale inapombidi (wakati wa kukuchombeza )....nini kinamfinya aziachie wakati huo kama sio amekuchoka?!Owkey unaweza ukampatia visingizio kibao kmf..alishindwa kujizuia na bla bla kibao...mara moja na mbili kisingizio kinaweza kumaliza tatizo ila inakuwaje pale anapoendelea na kurudia kitu kile kile mara nne tano huko?!
 
Mimi weakness yangu ni kuambiwa napendwa tu................................hata nikimfumania mara mia,akiomba msamaha na kuniambia ananipenda tu inatosha............NITAMUACHA PALE TU ATAKAPOSEMA KWA MDOMO WAKE HANIPENDI AU HANA HISIA NA MIMI TENA,MENGINE YOOOTE NI MAPUNGUFU YA KIBINADAMU TU AMBAYO I BELIEVE NO MAN IS IMMUNE TO THEM UNLESS THE WORD PERFECT IS A COMMON EXPRESSION OF EACH DEED!
 

Aiseeee...

Kwahiyo wewe uambiwe tu unapendwa haijalishi ni kweli au uongo?!
 
...kama hisia za kupenda zinapokuja kwa sababu mbali mbali, hisia za kuachana pia huja hivyo hivyo.. i.e Ugomvi wa mara kwa mara, kutukanana, kuacha/kunyimana tendo la ndoa, ulevi wa kupitiliza, kukata mawasiliano, cheating na Ex-/new partners, utoro [absentiism]nyumbani, na visa vingi vinginevyo..

Kwa ufupi, ni hisia zote ambazo ni kinyume na kupenda. La msingi ni kupambana na vishawishi hivyo ili kunusuru mapenzi/ndoa yako. Bahati mbaya/nzuri, wengi 'huanza kuachwa' hata kabla hawajaingia kwenye ndoa, lakini huzifungia macho makusudi dalili hizo kwa matumaini wakishaoana au kupata mtoto Wenza wao watabadilika. 'love is blind!'
 

Ahsante sana Mbu....
 
Lizzy,

Ma-Bachela na Ma-Single huwa mnanifurahisha sana! Mambo yenu ni ya kusadikika tu!

mie nimebaki naduwaa coz Lizzy alivyoviorodhesha ndivyo tunavyopambana navyo humu ndani kwa namna moja au nyingine...cheating/gubu...etc ndio hayo ya kila cku yanayotuzunguka....
 
Inaboa sana....

Kwenye masimango bado hujaambiwa kama sio mimi ungekua hivi au vile?!Ungejua hiki au kile?!Sijui nini na nini....

so kwa kauli kama hiyo hutaweza kuvumilia japo unajua aliku push kidogo kwa kuongezea jitihada zako ndio umefika hapo ulipo? yaani amesema tu kwa kujifariji/pombe etc?
 
so kwa kauli kama hiyo hutaweza kuvumilia japo unajua aliku push kidogo kwa kuongezea jitihada zako ndio umefika hapo ulipo? yaani amesema tu kwa kujifariji/pombe etc?


Kila siku jamani!?Hata mbele za watu bila au hata ukiwepo?!Kuna umuhimu gani wa kufanya hivyo kama asante nilishampa na sichoki kumuonyesha kwamba nashukuru kwa ukarimu na uwepo wake?!Baada ya muda mtu utakosa hata amani...hata akikupa kitu unaogopa kuchukua..kisa cha kuishi kwa wasiwasi?!
 
mimi hizo 2, 5 na 7
zitanichosha haraka sana
Halafu somo la uvumilivu inabidi nirisiti
 

unakuwa tangazo au refference, ya 'ukarimu' wake naichukia hii
 

mbali na gubu bado kuna mengineyo, binafc ckujuaga kama angeweza ku cheat kwa kiac kile, kwa nilivyokuwa namuamini, (nilichukulia yale mapenzi ya mwanzo ndio yataendelea hata baada ya miaka 5) kumbe hapana....kwa wakati ule ungeniuliza ningesema ctaweza kumsamehe..... amesha cheat na nikajaribu kusamehe na maisha yanaendelea japo inauma but nilikubali ukweli kwamba kimetokea na ckuwa tayari kwa wakati ule tutengane, so my dear Lizzy, ucpokutana na ki2ko hiki utakutana na kile, either cheating/gubu/kupigwa etc.....hakuna mkamilifu.
 
mie nimebaki naduwaa coz Lizzy alivyoviorodhesha ndivyo tunavyopambana navyo humu ndani kwa namna moja au nyingine...cheating/gubu...etc ndio hayo ya kila cku yanayotuzunguka....
<br />
<br />

Mae, mnaweza kuona ni mahusiano ya kufikirika zaidi.....

Nimesoma mambo yaliyoorodheshwa juu, nikajaribu kupima....hata ni ngumu japo inawezekana kabisa kuachana kutegemea na mtu na mtu.

Mimi nimefikiria hayo yanapofanywa repeatedly, unajua ni kwa kiasi gani yanaleta 'damage kwenye mahusiano kati ya wawili?

How long can one put up with such things?
 

Nyamayao,

Si wanawake tu, hata wanaume wanakutana na mambo mengi ya ajabu sana kwenye ndoa. Nadhani hawa vijana wanataka tuwatishe waweke mpira kwapani kabla ya hata mechi kuanza.

Nawashauri watulize boli na wajiandae kukabiliana na hali yoyote ile itakayojjitokeza mbele yao.
 

so point hapa ni kwamba yafanyike mara moja moja ndio mtu anaweza kuvumilia? mnajua kila binadamu ana mapungufu yake? unajua kuna wakati binadamu alivyi ndivyo alivyo huwezi kumbadilisha? hayo yapo sana humu ndani tunachofanya ukiona yamekuzidi we jipangue tu but mcdhani ha2yapitii baadhi ya hayo kwa namna moja au nyingine..tunayapitia sana ishu ni kwamba ukiona yamezidi unajipangua tu.
 

unalalamikia kupigwa? wenzako wanamwagiwa maji ya moto na sku ya pili wanaomba razi wao!

Halaf hizo nyengine ulizotaja zote ndio mahusiano yenyewe, sasa kama huwezi hizo nakushauri uokoke tu Miss Unga Ltd
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…