Ni kitu kipi unatamani kumwambia mtu unahisi utapata relief

Ni kitu kipi unatamani kumwambia mtu unahisi utapata relief

Utawala2025

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2023
Posts
1,144
Reaction score
2,755
Habari.

Ni nyakati zipi ngumu unapitia kwa sasa unatamani ufungue moyo upate mtu mmoja umueleze yanayokusibu ulie sana ,unyamaze halfu ije idea mpya yenye kusolve shida yako.

Tuambie; Kipi unachopitia kwa sasa unatamani umwambie mtu mmoja awe karibu akusaidie pekee umechoka.
 
Changamoto zinatofautiana, kila mmoja anapewa au anakutana nazo kulingana na uweza wake au kwa kipindi fulani.
Mtu anaweza kusema anayopitia wewe msikilizaji ukaona mbona kama ni kitu kidogo sana ! Lakini kumbe kwake ni kikubwa mno.

Ila yote ya yote pito lolote apitalo mtu ajue ni kwa wakati tu, na wakati si wa milele , wakati haudumu, kesho iliyo na mabadiliko haipo mbali, na ukiona giza au usiku umekuwa mkubwa sana ujue asubuhi imekaribia sana.
 
Namshukuru Mungu hadi hapa nilipofikia nna uwezo wa kuyakabili yote yanayonikumba. Na hii ni kwa sababu nilishakubali kuwa yote ni sehemu ya maisha. Kila kinachotokea na kuendelea ni sehemu ya maisha.
 
Nashukuru Mungu mapito yangu yamebaki story
 
Back
Top Bottom