Changamoto zinatofautiana, kila mmoja anapewa au anakutana nazo kulingana na uweza wake au kwa kipindi fulani.
Mtu anaweza kusema anayopitia wewe msikilizaji ukaona mbona kama ni kitu kidogo sana ! Lakini kumbe kwake ni kikubwa mno.
Ila yote ya yote pito lolote apitalo mtu ajue ni kwa wakati tu, na wakati si wa milele , wakati haudumu, kesho iliyo na mabadiliko haipo mbali, na ukiona giza au usiku umekuwa mkubwa sana ujue asubuhi imekaribia sana.