Ni kituko gani cha ugomvi ama ngumi hutokisahau?

Katika timu ya watoto ya mtaani kwetu mimi nilikua kapteni. Sura mbaya, mfupi, mweusi, nimekomaa, mkali basi wananiit Mourinho (niliokua nao wananiita hili jina bado)

Wapinzani wetu wakubwa walikua wanatokea eneo linaitwa Msikitini kwahiyo ilikua tunawaita watoto wa msikinitini. Tulikua tunacheza nao mechi mara kwa mara, katika game zaidi ya 100 tumeshinda zaidi ya 70. Siku hiyo wakaja na mchezaji mpya anaitwa Tizo, kijeba kimekomaa hatari mi naonekana wa kawaida (hiyo Tizo ni kifupi kumbe anaitwa Matatizo)

Basi tukawafunga kama kawaida wakaanza rafu mi nikawabonda naona Tizo ananikimbilia kabla sijamshona raia wakaingilia, tukakubaliana tukutane hapo uwanjani usiku anatoka mtu wa upande huu anamchagua wa upande ule wanakiwasha.

Mida ikafika tukatokea, kufika akaanza mtu kutoka timu yangu tulikua tunamuita Diblo, akamchagua mtu wake akamshona vizuri tu. Kisha Tizo kutoka kwao akanichagua mimi.

Moyo ulipiga 'Paaa' ila sasa mimi ndo Mourinho sitakiwi kuhofia nikavua ndala na shati nikasogea kati, kama umeona muvi ya In the Streets Only the Strong (Almaarufu Paranawe) kile kiduara walichokiweka na sisi tuliweka kama hicho.

Kuzama kati bwana Tizo alivyofika tu akanishika shati kwa mkono wa kulia halafu wa kushoto anatembeza vitasa tu, yaani Tizo hataki shida, hataki uende mbali anataka akiwa anakushona uwe hapo hapo.

Sasa kile kiwewe kikampa advantage ya kunibomonda ngumi tano za fasta fasta mi nikareact kwa kumkata mtama, sasa si kanishika shati? Tukaenda chini wote dadeq yaani tunaanguka ila Tizo anarusha tu ngumi na ngumi zote zinatua kwenye shavu.

Kufika chini nikamkalia juu nikaanza kupeleka vitasa visivyo na idadi, nikasikia za juu juu, za juu juu nikaona mingo yangu imekufa maana pale chini ushindi ulikua huu hapa.

Tukainuliwa.

Kama kawaida kufika tu bwana Tizo kakimbilia shati kwa mkono wa kulia wa kushoto anaachia vitasa tu. Kumkata mtama siyo option tena maana raia washasema za juu juu.

Nikainama nikaanza kumpelekea body shots, nasikia 'Muoneni Tizo anaruka' yaani ilikua kila body shot ikitua bwana Tizo anaruka na kanishika shati bado muda huo ila kwavile nimeinama inakua haiwezekani kunifikia, kwahiyo mi nikawa nafaidi tu kuachia body shots bila upinzani.

Pambano likafa baada ya askari maarufu wa kwa Kopa kuingilia kati na kututimua (alikua anaitwa Afande Sura Mbaya)
Nilishukuru uwepo wake kwakweli, tulitoka mbio ndala zangu nikaletewa na team mate.

Sasa washkaji wananisifia ile dah Mourinho wewe hatari kila ukipeleka ngumi jamaa alikua anarudi nyuma, wananisifia lakini nikijaribu kuongea siwezi, mdomo haujiachii, nikanyanyuka naondoka chozi hilo linatoka, taya ilichezewa hadi kutafuna nilishindwa siku hiyo.

Huyo Tizo hadi leo hatuongei.
 
Mimi sijawahi shindwa pambano utotoni nashukuru kuwa yangu yote sijwahi kuonewa nina kamwili afu nikikasilika mtu tu anaogopa atomatic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…