Ni kivipi Rais Samia Suluhu asingevunja Katiba?

Ni kivipi Rais Samia Suluhu asingevunja Katiba?

Pslmp

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2021
Posts
1,622
Reaction score
2,458
Matamanio ya wengi, hasa upande wa Upinzani Kupitia Chama cha Chadema kupitia mgogoro mkubwa wa wabunge wake waliofukuzwa uanachama na kukosa sifa ya kuwa wanachama wa Chama hicho na moja Kwa moja kukosa uhalali wa kuwa wabunge.. wengi wao walitegemea Mh Raisi akalikemee Jambo Hilo bungeni katika hotuba yake ya Jana,

Wengine wakienda mbali zaidi kusema, mh Raisi Angelitoa amri ya kufukuzwa hao wabunge kwa maana ya kwamba, wako kinyume na katiba, ni Kweli wako kinyume cha katiba, Je Raisi akiingilia Hilo yeye hawi kinyume cha katiba?

Mimi nataka kujifunza hapa, Ni kivipi Mh Raisi wetu asingevunja katiba?

Bunge, ni mhimili unaojitegeme, inakuweje matarajio ya wanachadema watamani Raisi aingilie mhimili mwingine? Sio kinyume cha katiba?

Kama ndivyo, Ni nini kifanyike kuhusu swala hili la wabunge waliokosa uhalali...!

Wataalamu wa Sheria...! Sheria inasemaje hapo
 
Back
Top Bottom