Ni kiwango kipi sahihi cha matumizi ya kitunguu swaumu kwa kuimarisha kinga ya mwili?

Bullshit

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
1,357
Reaction score
1,596
Habari zenu wana JF na poleni kwa majukumu

Kutokana na JF kuwa msaada wa maarifa kwangu ndomana nipatapo jambo au kutatizwa na kitu fulani basi bila shaka huwa kimbilio langu.

Wapendwa mimi ni mpenzi sana na ninapenda sana kutumia kitunguu swaumu kila siku nikichanganya na kikombe kimoja cha maziwa.
Huwa natumia hata kete kumi kwa siku hapo ni baada ya kuvikatakata vizuri vipande vidogo naweka kwenye maziwa natumia. Hii ni kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.

Tatizo langu ni kuwa nadhani nakosea kiwango ninachotumia. Nina wasiwasi natumia kiasi kikubwa kwa siku na nahofia naweza kupata mafhara hapo baadaye.

Maswali:
Je, kiwango sahihi ni kipi?

Kuna madhara gani kutumia kitunguu swaumu kupita kiasi?

Kitaalamu ni sahihi kutumia kitunguu swaumu kila siku au ni kwa muda fulani tu?

Nitashukuru kwa mchango wako
 
hata mimi mkuu hii kitu nimekua addicted nacho sasa alafu nilianza kama utani tu...sema mimi ninatafuna hivyo hivyo nameza bila kuchanganya kwenye kinywaji chochote na kwa siku naweza kumaliza vitungu swaumu viwili vizima
 
hata mimi mkuu hii kitu nimekua addicted nacho sasa alafu nilianza kama utani tu...sema mimi ninatafuna hivyo hivyo nameza bila kuchanganya kwenye kinywaji chochote na kwa siku naweza kumaliza vitungu swaumu viwili vizima
khaaa na kilivo na harufu sasa si mdomo utakua unanuka sana
 
Aisee kwani vinasaidia nini wakuu? [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…