Maalim Jumar
JF-Expert Member
- Dec 28, 2010
- 1,259
- 118
Naulisa hivi hayo maneno mawili ndivyo sawa sawa kuyatumia katika hizo sentesi?Sijaelewa vizuri unachouliza hapa ndugu yangu...
Wanafanyana= kudaiana.'anajidai'
Ka'mie hivyo hivyo....Kusikia nishasikia sana tu...
Nilikua namaanisha huenda wameyatafsiri hayo maneno kutoka kizungu kuyaleta katika swahili.Ni kizungu au kiswahili?
salaam jf!
Haya maneno nimekua nikisikia mara kwa mara yakifikisha ujumbe.
Je ni sahihi?
1-anajitia (huyu kaka anajitia haelewi).
2-anajifanya (huyu msimamizi anajifanya haoni).
3-.................
4-..................
Hua yanishangaza sana yanavyotumiwa.
Umewahi kusikia sentensi zingine kama hizo?
Nawakilsha kwenu !
sijaelewa vizuri unachouliza hapa ndugu yangu...
Je kutiwa?Kujiita maana yake jina husika si lile ulilopewa na wazazi wako. Ni jina unalojipa mwenye kwa sababu ya umaarufu, au shughuli yako au tuseme mapenzi yako. Haya majina yenye sifa ya "kujiita" unayakuta sana kati ya wanamuziki,macelebrities wa filamu na kwenye social networks ambako watu hawatumii majina yao halisi bali wanajipa majina ya bandia, wanajiita.... Kwa hiyo"kujiita" si tafsiri kutoka Kiingereza vinginevo unamaanisha kitu kingine.
Vivo hivo "kujifanya" ni kiswahili kamili kabisa. Kujifanya maana niku-act, kufanya usanii, kuvaa utu au nafsi isiyo yako. Maana yake unajionesha kile usichokuwa. Kwa hiyo "unajifanya." Yaani katika uhalisia wako wewe huko hivo, bali unataka kutuaminisha kwamba uko hivo. Unajifanya.