Ni Kombani, Werema (Star tv) & Wassira, Nape (TBC)

jamani wengine tuko vichochoroni mtujuze kwa undani nini kinaendelea na vilaza wetu werema na kombani
 
Wadau..Waziri Wassira na Mwanasheria Mkuu Werema wapo TBC1 sasa hivi wanajadili Katiba...!Wenye access na TV twende tuangalie..!
 
nani wasira aaaaaaaaah, Naogopa kuttune TV kwenda TBC maana mwanangu ataota ndoto za kutisha.
 
kama unataka kutapika wasikilize hao vilaza....
 
Wassira anasema ni sawa kwa Rais kuandaa kila kitu mfano Hadidu za rejea.,kuunda tume, kuunda Bunge la Katiba..,anadai eti watanzania wana mwamini na ndio maana walimchagua mwaka jana..!

Werema anakili kwamba Wanzanzibar hawakushirikiswa wakati wa uandaaji wa Muswada wa Katiba..!
 
huyo mtangazaji vipi, mbona wasira anapiga soga mpaka kaamua kutoka nje ya mada ye katulia tu, kawa msikilizaji?
 
..kwanza tunaambiwa hisa za Zanzibar ktk kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania BOT zilikuwa ni 12%??

..baada ya hapo Zanzibar ikaenda kuanzisha People's Bank of Zanzibar ambayo ilikuwa ndiyo "benki kuu" ya Zanzibar mpaka mwaka 2001 walipokubali kutumia Benki Kuu ya Tanzania [BOT].

..jumping a few steps ahead, kuna suala la Zanzibar kupewa asilimia 4.5% ya mapato ya serikali ya muungano. je, formula hii ilipatikana vipi? na mgao huu ulianza lini?

..halafu kuna suala la TRA. kabla ya kuanzishwa kwa chombo hiki mwaka 1995/96 ni chombo gani kilikuwa kinakusanya mapato Zanzibar? je, Zanzibar ilikuwa inakusanya mapato yake yenyewe na kuyatumia wenyewe bila kuingiliwa na serikali ya muungano?

..kama PBZ ilikuwa ndiyo benki kuu ya Zanzibar mpaka mwaka 2001, je ina maana tangu 1966 to 2001 Zanzibar ilikuwa na uwezo wa kukopa nje ya nchi bila udhamini wa serikali ya muungano?

..je, ni kwanini Zanzibar ikaamua kuachana na People Bank of Zanzibar na kuamua kuwa mshirika kamili ktk Bank of Tanzania? Ni nini hasara na faida za uamuzi huo? wakati wa uchaguzi Maalim Seif aliulizwa kama akipewa madaraka ataanzisha Benki Kuu ya Zanzibar akakataa.!!

..je, ni makosa kudai kwamba Zanzibar imekuwa ikiendesha uchumi wake yenyewe toka mapinduzi mpaka miaka ya [96 -- 2001] kwasababu walikuwa na Benki Kuu yao wenyewe, na mamlaka yao ya kukusanya mapato?


..nanukuu maelezo ya Othman Masoud Othman ambaye ni mwanasheria mkuu wa Zanzibar kuhusu PBZ na BOT


..hapa Bw.Othman Mahmoud Othman anazungumzia kidogo kuhusu masuala ya kodi ya mapato na matumizi yake.

 
Eti, swala la muungano ni swala nyeti, sio la kujadili kwenye mjadala wa katiba mpya!
 
Sakata la kuundwa kwa Katiba mpya limeanza kuchukua sura mpya, baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti nchini (RAAWU), kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema kujiuzulu mara moja nafasi yake.

RAAWU kimemtaka Werema aondoke mara moja katika utumishi wake huo wa kisheria ndani ya Serikali, kwa kile kilichoelezwa kwamba anatetea miswada mibovu inayominya uhuru na fursa ya wananchi kutoa mawazo yao katika uundwaji wa katiba mpya ya nchi.

Mbali na Werema, chama hicho pia kimetaka Rais apunguziwe madaraka aliyonayo katika nchi, ili kutoa nafasi kwa mamlaka nyingine kuwa na nguvu za kimaamuzi, na kufanya hivyo ni kuliondoa taifa katika utawala na maamuzi ya kutegema kiongozi mmoja.

Katibu wa RAAWU Kanda ya Ziwa, Ramadhani Mwendwa ameyasema hayo jana Mwanza, wakati alipokuwa akizungumza na NIPASHE Jumapili kwa njia ya simu, juu ya hali na mwenendo wa nchi, hususani matatizo yanayowakabili wafanyakazi na masuala ya uundwaji wa katiba mpya.

Mwendwa amesema kwamba, hivi sasa taifa lipo katika masuala ya uundwaji wa katiba mpya ambayo wananchi wanaihitaji, na kwamba katika sakata hilo Mwanasheria Mkuu wa serikali, ameonekana kuegemea zaidi katika matakwa na mawazo ya watawala juu ya uundwaji wa katiba na kuacha kusikiliza kilio kikubwa cha Watanzania.

Alisema, Werema anapaswa kuishauri vizuri serikali katika mambo mazito kama haya ya uundwaji wa katiba mpya, ikiwa ni pamoja na kufuata na kuzingatia matakwa ya wananchi wenyewe na si mawazo na matakwa ya watawala ambao wanaonekana kutaka katiba yenye mianya ya kuwepo kwa maslahi yao binafsi.

Akizungumzia suala la Rais wa nchi kupunguziwa madaraka, Mwendwa alisema kwamba ni lazima ifike sehemu rais apunguziwe mamlaka, na kwamba siyo kila jambo mpaka aamue raia mwenyewe.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Kama ameharibu mswada wa sheria wakati akijua nini wananchi wanataka na kwenda kinyume chake tutegemee nini atafanyia mabadiliko? Afadhali ajiuzuri na aje mwingine mwenye kulenga maoni ya wananchi
 
Hivi kweli Werema alikuwa Jaji? Je kuna watu walionyongwa kutokana na hukumu iliyotolewa na Werema? Kama kuna mtu ana ndugu aliyenyongwa kutokana na hukumu ya huyu jamaa, basi ajue kuwa huenda alimpoteza ndugu yake huyo bila sababu yoyote bali ukilaza wa Werema.
 

ndugu yangu kichuguu huyo werema hafanyi hivyo kwa ukilaza anafanya makusudi akiwa anajua kuwa sio sahihi. Hapo alikaa na wanasiasa wakadraft mswada mbovu ili walinde maslahi yao
 
Sakata la kuundwa kwa Katiba mpya limeanza kuchukua sura mpya, baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti nchini (RAAWU)....

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Researchers, Academicians and Allied Workers Union
 
Mwanzoni nilifikiri mtu akipewa cheo cha "Urais, Uwaziri, Mwanasheria Mkuu, Jaji, IJP, Mwendesha Mashtaka, na cheo chochote Serikalini au kwenye taasisi za kidini" nilikuwa naamini kuwa mtu huyo anafanya ile kazi kwa mujibu wa haki kwa kutumia elimu yake kwa manufaa ya Taifa.

Kumbe nilikuwa najidanganya tu, vyeo hivyo vinaweza kushikwa na mtu yeyote wakimo, "wezi, majambazi, vyangudoa, mafisadi, walafi wa mali ya umma, wauaji, wenye visasi, wanafiki, waongo, vibaka, madalali, wachawi, na wengine wenye sifa kama hizo" Nimejionea kwa hakika ndani ya Serikali yetu na zingine za kiafrika!

Sina imani nao kabisa watu wanao onyesha waziwazi sifa hizi kama Werema afanyavyo. Hafai kabisa, simtofautishi na Chenge!
 

Kumbuka wiki iliyopita bungeni alivyoendeshwa na Mheshimiwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu lisu jinsi Werema anavyoenda kinyume cha sheria kwa kutaka ushauri wa mahakama uwe mikononi mwa makada wa ciciem
 
walema akijiuzulu huyo mwingine atateuliwa na nani? niyaleyale walema si kwamba hajuwi wajibu wake anayafanya hayo kwa matakwa ya mutu&kindi fulani kuyafuta yote haya ni katiba mpya tuu tukomae juu ya katiba
 
Hilo la Benki Kuu, TRA sijui na nini vile ni mwendelezo wa wanzanzibar kujikomboa toka ukoloni mamboleo. Wazanzibar hawawezi kupata Central Bank yao wala kupata Revenue Authority ya kwao hadi pale viongozi wao watatokana na wao wenyewe na sio kutokea Dodoma au penginepo popote Tanganyika(kama ilivyo kwa sasa). Ni lini wazanzibar walimpata kiongozi waliyemtaka?

Katiba mliojitungia wenyewe ni kiashiria kizuri kuelekea ukombozi kamili wa wazanzibar. Na hata muungano uwe ule wanaoutaka wazanzibar wote. Usiwe huu unaolindwa na kufunikwafunikwa na viongozi wanapitishwa kule Dodoma na kuaswa kwamba wahakikishe muungano haujadiliwi na wazanzibar.
 
Ndiye wa kwanza kumwambia spika amuondoe Mbunge wa Nyamagana bungeni eti katukana bunge!

Nadhani jamaa ufahamu wa sheria ni unga Robo. Anahangaika na shibe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…