Ni kosa kubwa leo hii Kagame kutumia Genocide kama kisingizio cha kusema na kufanya anachotaka

Ni kosa kubwa leo hii Kagame kutumia Genocide kama kisingizio cha kusema na kufanya anachotaka

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Wanajamii, nisaidieni kufikisha ujumbe huu kwa Kagame na viongozi wa Rwanda.


Hadi sasa najiuliza Raisi wa Kagame na baadhi ya mawaziri wake waliwezaje kuropoka maneno waliyosema pale ambapo raisi wa Tanzania aliposhauri Rwanda iongee na wapinzani wa FDLR.

Kuna mtu aliwahi kusema Kagame ana matatizo ya kisaikolojia (pia mental instability), kutokana na namna yake ya ukuzi ikiwa pamoja na kufiwa baba yake mzazi mapema katika maisha yake na kuwa na umbile dogo sana ambalo hakulipenda. Labda ni kweli.

Kwangu mimi naona tatizo kubwa la Kagame ni moja; kwamba anathibitisha kwa kila aina kwamba common sense is not common to everyone - na Kagame lacks common sense in a big way.

Hatukatai kwamba Genocide ya Rwanda was one of the most painful things to ever happen - sawa tu na Holocaust kule Ujererumani, au apartheid brutality kule South Africa. Na pia it was so regrettable Jumuiya ya Kimataifa haikuwasaidia Watusi waliokuwa wanauwawa mapema kama ilivyobidi.

Lakini Kagame hapaswi kutumia Genocide kama right ya kusema anachotaka na kufanya anachotaka, na kudhani Genocide inampa haki ya ku-dictate anachotaka kwa Rwanda na nchi nyingine.

Mwana saikolojia yeyote atakuambia kwamba Kagame anatumia Genocide kama ticket ya kuwa na utawala wa kibabe, kukandamiza upinzani, kuweka watu mahabusu bila sababu, kupiga kelele (tantrums) kila anapokosolewa! Anatumia genocide kujaribu kugenerate guilty feelings kwa wengine na kujifanya yeye ni innocent victim. Kagame aelewe wengi wetu hatudhani yeye ni innocent victim wa genocide.

Yaani ukimgusa tu Kagame - anapiga kelele - Genocide! Genocide! Hamkutusaidia! Hamkusaidia! Msituingilie! Msituingilie! Wewe ni genocide perpetrators sympathizer!

Leo hii huko Rwanda unaweza kufungwa kwa kutaja neno genocide tofauti na Kagame anavyotaka ikumbukwe!

Hizo, kwa kifupi ni tantrums za kitoto mbazo mtu wa umri wa Kagame hapaswi kuzionyesha miaka 20 baada ya Genocide. Kwa ufupi, Kagame anakuwa kama spoilt child ambaye kwa sababu aliumia kidole labda miezi miwili iliyopopita hataki aguswe kwa kisingizio kuwa ana kidonda!

Kwanza tujiulize - hivi ni kweli Tanzania haistahili kusema lolote juu ya suala la amani linayoihusu Rwanda? Je Kagame amesahau kwamba hata chanzo cha Genocide Rwanda ni safari ya raisi wa Rwanda wakati huo akitokea Tanzania kwa madhumuni ya amani? Je Kagame anasahau kwamba kimbilio kubwa la Watsi wakati wa Genocide ilikuwa ni Tanzania - ambayo wakati huo ikafikisha rekodi ya dunia ya kuwa na idadi kubwa ya wakimbizi kwa wakati mmoja?

Hivi Kagame anafikiri Tanzania inapenda kuwa na wakimbizi toka Rwanda kila baada ya miaka kadhaa? Je amesahau kuwa Tanzania mara nyingi imekubali gharama za kuwa na wakimbizi toka Rwanda, kuwasomesha na hata kuwapa uhuru wa kuwa Watanzania ikiwa tu wataukana uraia wao wa Rwanda? Je amesahau kuwa baadhi ya mawaziri wake na viongozi wake leo hii walisomeshwa bure na Tanzania na sasa wanachangia kuijenga Rwanda? Je, haoni kwamba yote haya yanaipa nafasi Tanzania kutoa ushauri juu ya amani ya kudumu huko Rwanda?

Kama hakupenda ushauri toka kwa JK wa Tanzania, kwa nini asishukuru na kuukataa kidiplomasia? Je mtu anaepiga kelele na kutukana pale anapopewa ushauri unaokubalika na wengine wengi, si dalili kwamba kweli ana matatizo ya kisaikolojia na huenda hata mental instability?

Kagame anapaswa kujua kwamba kwa Tanzania, suala la Wanyarwanda kukimbia nchi yao na kuja Tanzania haliangalii nani huko Rwanda yuko sahihi - Kagame au FDLR. Tanzania inachojali ni kwamba kusitokee machafuko mengine yatakayoumiza raia wa Rwanda na Tanzania- whether Kagame ana sababu za msingi za kuwachukia FDLR au la. Na pia Tanzania inaangalia kwamba kuwe na suluhisho lenye kuzaa matunda. Wanaoumia katika mgogoro wa Kagame na FDLR ni Warwanda wa kawaida, wala si Kagame. Kwanza Kagame hata huko vitani kupigana na FDLR haendi. Anakaa ofisini na kukubali innocent victims waendelee kuumia kwa msimamo wake usio na kichwa wala miguu juu ya FDLR. Machafuko yakitokea Rwanda leo hii, Kagame hatawazuia Wanyarwanda kukimbilia Tanzania ili kuokoa uhai wao.

Si mara zote nakubaliana na sera za JK, lakini kwa hili la Rwanda, ningependa nimshauri JK ampuuze Kagame, na akumbuke kwamba Nyerere wa Tanzania, ilibidi wakati fulani atukanwe na baadhi ya viongozi wa ANC kwa ajili ya kuwashawishi wakubali kuongea na Makaburu. Maongezi hayo ndio yaliyoletelea Afrika Kusini leo hii kujiita Rainbow nation - kwamba inaundwa na weusi, weupe, na wenye rangi mchanganyiko!

Na je, Kagame anasahau kwamba japo maovu ya kutisha yaliyofanywa na wazungu dhidi ya weusi bado kina Mandela walikubali kukaa nao na kuongelea amani? Ukweli ni kwamba wengi wa Makaburu waliowaumiza weusi hadi leo hii wapo mitaani Afrika Kusini - kwa kuwa weusi wa Afrika Kusini wamekubali yaishe. Hiki ndicho kilichompa umaarufu Mandela - kukubali yaishe.

Sasa yeye Kagame ni nani ambaye kwake mambo ni tofauti sana hawezi kukubali yaishe? Je ile Genocide ya Rwanda inauma sana kuliko Holocaust ya Wanazi, kuliko Apartheid ya South Afrika, kuliko UNITA ya Angola, RENAMO, IRA ya Uingereza, nk?

Genocide ilitokea karibu miaka 20 iliyopita - Huenda hata wengi wa wa wapiganaji wa FDLR leo hii hawakushiriki katika genocide - sasa kwa nini Kagame anataka kuhukumu watoto kwa makosa ya baba zao?

Anachofanya Kagame ni sawa na kusema leo hii Wa -Israel wawachukie Wajerumani kwa ajili ya Holocaust. Je Kagame amesahau ilichukua muda mfupi sana kwa Waisrael kutowahukumu Wajerumani wote kwa maovu dhidi yao? Msumbiji wawachukie RENAMO? Uingereza wawachukie IRA, nk?

Ikiwa Kagame ana watu specific katika FDLR ambao anaona wanastahili kufikishwa katika vyombo vya sheria - basi aliweke hilo wazi, kwa kuwa hata ICC inakubaliana nalo. Lakini leo hii, miaka 20 baada ya genocide, kusema kila mtu aliye FDLR ni mbaya na Kagame hawezi kuongea naye juu ya amani - huko ni kuonyesha kwamba Kagame bado ana tatizo kubwa sana na kisaikolojia na ana behave kama a spoilt child ambae hadi leo hajakua.

Ushauri wa bure kwa Kagame - na akitaka anitukane na mimi; Kagame kama una nguvu pigana na umasikini Rwanda, sio kuelekeza nguvu nyingi kwenye vita. Hela nyingi unazotumia katika kampeni dhidi ya FDLR fikiria ikiwa zingeelekezwa kuboresha afya na elimu Rwanda hali ingekuwaje.
 
Hapo kwenye red: Kagame hana uchungu na hiyo pesa kwani haitokani na kodi za Wanyarwanda. Gharama ya vita inayopiganwa na Rwanda huko Eastern DRC inatokana na madini wanayoiba huko huko. SADC waongeze majeshi Eastern DRC hasa hasa kwenye mpaka wa DRC-Rwanda ili kuzuia wizi wa madini, automatically jeuri yake itapungua kama siyo kwisha kabisa.

Licha ya kwamba jeuri ya Kagame inatokana na malezi aliyopata utotoni, pia raisi mstaafu wa 43 wa Marekani, Bill Clinton, amechangia kuimarisha ujeuri wa huyo jamaa kutokana misaada aliyoitoa kwa RPF kabla na hata baada ya kukamata madaraka nchini Rwanda mwaka 1994. BIll Clinton, Collin Powel, Madelline Albright, n.k. wakati wa utawala wao lengo lao kuu lilikuwa kuhitimisha ushawishi wa Ufaransa katika nchi ya Zaire ili wafaidi lasilimali zake.

Ili kufanikisha azima hiyo ilikuwa ni lazima watafute nchi jirani na Zaire waitumie kuanzisha mashambulizi dhidi ya himaya ya Ufaransa (Zaire), hivyo wakamfuata raisi Habyalimana wa Rwanda ambaye alikataa kumsaliti rafiki yake wa karibu na wa siku nyingi, Frocoise Miterrand wa Ufaransa. Bill Clinton akaamua kumuunga mkono Kagame (RPF) kwa kushirikiana na Museveni na kupanga njama za kumuua raisi Habyalimana na kufanikiwa usiku wa kuamkia April 6, 1994.

Walijua madhara (reaction) itakayotokana na mauaji dhidi ya raisi Habyalimana lakini walipuuza maana walikadiria kuwa idadi ya watu watakaokufa kutokana na kulipiza kisasi cha mauaji hayo isingezidi 50,000 wakajifariji kuwa hiyo ni idadi reasonable kwani ni kawaida baadhi ya watu kufa kama kafara especially unapotaka kutimiza lengo kuu na muhimu.

Kagame is not worth to regard himself innocent, he is not! Damu ya Wanyarwanda aliowatoa kafara inamlilia usiku na mchana, hatakuwa na amani kamwe moyoni mwake na ushahidi ni jazba anazoonesha.
 
Damu ya Wanyarwanda aliowatoa kafara inamlilia usiku na mchana, hatakuwa na amani kamwe moyoni mwake na ushahidi ni jazba anazoonesha.

Kwa hili la jazba nimelisikia sana, ambayo inaonyesha namna fulani ya mental instability kama nilivyosema. Ni hatari sana kuwa na kiongozi wa nchi mwenye mental issues.

Lakini kwa Rwanda, nani atamfunga paka kengere? Imagine uko Rwanda na unapendekeza kwamba Kagame akafanyiwe tests kuhusu mental status yake!
 
Ohhh pls...hii cinema tumeshaiona na hakuna jipya hapo,naona mmepata ubao mpya JF to advance your agenda of hate and ant ant Kagame,moderators wako wapi kuruhusu huu upuuzi?
 
Kwa hili la jazba nimelisikia sana, ambayo inaonyesha namna fulani ya mental instability kama nilivyosema. Ni hatari sana kuwa na kiongozi wa nchi mwenye mental issues.

Lakini kwa Rwanda, nani atamfunga paka kengere? Imagine uko Rwanda na unapendekeza kwamba Kagame akafanyiwe tests kuhusu mental status yake!
Kagame ni kama mfalme Nebukadneza wa iliyokuwa Babiloni, anayempinga nchini mwake anajuta kwa nini alizaliwa. Huyu jamaa nchini Rwanda ni mungu-mtu usipime!
 
Hapo kwenye red: Kagame hana uchungu na hiyo pesa kwani haitokani na kodi za Wanyarwanda. Gharama ya vita inayopiganwa na Rwanda huko Eastern DRC inatokana na madini wanayoiba huko huko. SADC waongeze majeshi Eastern DRC hasa hasa kwenye mpaka wa DRC-Rwanda ili kuzuia wizi wa madini, automatically jeuri yake itapungua kama siyo kwisha kabisa. Licha ya kwamba jeuri ya Kagame inatokana na malezi aliyopata utotoni, pia raisi mstaafu wa 43 wa Marekani, Bill Clinton, amechangia kuimarisha ujeuri wa huyo jamaa kutokana misaada aliyoitoa kwa RPF kabla na hata baada ya kukamata madaraka nchini Rwanda mwaka 1994. BIll Clinton, Collin Powel, Madelline Albright, n.k. wakati wa utawala wao lengo lao kuu lilikuwa kuhitimisha ushawishi wa Ufaransa katika nchi ya Zaire ili wafaidi lasilimali zake. Ili kufanikisha azima hiyo ilikuwa ni lazima watafute nchi jirani na Zaire waitumie kuanzisha mashambulizi dhidi ya himaya ya Ufaransa (Zaire), hivyo wakamfuata raisi Habyalimana wa Rwanda ambaye alikataa kumsaliti rafiki yake wa karibu na wa siku nyingi, Frocoise Miterrand wa Ufaransa. Bill Clinton akaamua kumuunga mkono Kagame (RPF) kwa kushirikiana na Museveni na kupanga njama za kumuua raisi Habyalimana na kufanikiwa usiku wa kuamkia April 6, 1994. Walijua madhara (reaction) itakayotokana na mauaji dhidi ya raisi Habyalimana lakini walipuuza maana walikadiria kuwa idadi ya watu watakaokufa kutokana na kulipiza kisasi cha mauaji hayo isingezidi 50,000 wakajifariji kuwa hiyo ni idadi reasonable kwani ni kawaida baadhi ya watu kufa kama kafara especially unapotaka kutimiza lengo kuu na muhimu. Kagame is not worth to regard himself innocent, he is not! Damu ya Wanyarwanda aliowatoa kafara inamlilia usiku na mchana, hatakuwa na amani kamwe moyoni mwake na ushahidi ni jazba anazoonesha.

Umechambua vizuri sana hili la Kagame na ushiriki wake kwenye genocide, Kagame na RPF ndiyo waliofanya mauaji ya kutisha kuliko walivofanya Forces Armées Rwandaises (ex-FAR).Kwanza ikumbukwe kuwa Forces Armées Rwandaises (ex-FAR) walikuwa wanajilinda thidi ya uvamizi wa RPF katika nchi yao.Lakini hata hivo kuna msemo unasema kuwa mshindi hushinda pale anapokuwa ameuwa zaidi kuliko alieshindwa kwa hiyo RPF waliua watu kuliko walivoua Forces Armées Rwandaises (ex-FAR)
 
Kuna mtu aliwahi kusema Kagame ana matatizo ya kisaikolojia (pia mental instability), kutokana na namna yake ya ukuzi ikiwa pamoja na kufiwa baba yake mzazi mapema katika maisha yake na kuwa na umbile dogo sana ambalo hakulipenda. Labda ni kweli.

Mkuu Synthesizer umekusia jambo la msingi sana.

Kama ikatokea unacheza na watoto wenzako mtaani, kisha ukaharibu kimpira mlichokuwa mnachezea hatimaye kundi kama la watoto ishirini ... wakawa wanakukimbiza wakukamate wakushambulie kama adhabu ya makosa yako... !

Lakini ikatokea ghafla wakiwa karibu kabisa kukukamata Baba yako mzazi akatokea ukamrukia, ukamdaka na kukumbatia, Utajisikiaje ... Inakuwa kama umeondolewa mzigo mkubwa sana, hata pumzi na mapigo ya moyo yatarejea kwenye hali ya kawaida. Kikubwa zaidi shaka, woga, wasiwasi na hisia hasi (negative emotions) nyingine zinatoweka. Yaani Baba Mzazi anakuwa amezitowesha hizo negative emotions na kuwa eliminated na unajisikia huru kabisa. Ndio maana Baba anachukulia kama msingi na nguzo ya kile kinachoitwa Good Emotional Intelligence kwa mtoto.

Mtoto aliyelelewa na Baba mzuri, ameepushwa na mzigo mkubwa wa kubeba woga, shaka, hasira, chuki, kinyongo nk kwani uwepo wa Baba ni sawa na kuondoa hisia hizo kwa mtoto. Kwa hiyo ni rahisi kumgundua mtoto asiye na Baba anayemjali, Baba mkali kupitiliza, Baba asiye na mapenzi au Baba kutokuwepo kabisa nk. Yaani rahisi kabisa kuona ombwe la Baba kwa mtoto au Mtu mzima

Watoto wengine wanatokea kuzibeba hali hizo za Shaka, Woga, Hasira, Vinyongo nk hadi wanakuwa watu wazima kabisa na kueleleza hali hizo kwenye familia zao, sehemu za kazi kwenye jamii na pengine kwenye ngazi ya Taifa.

Kagame si tu kuwa amesheheni negative emotions zinazo mpelekea ubutu mkubwa wa kuwa na good emotional intelligence hasa inapokuwa ni kwenye uongozi. (Google thamani ya "emotional intelligence in leadership" ) bali yeye kujichukia na kutojikubali kimaumbile hii inapigilia msumari na inazidi kumteketezea uwezo wake wa Emotional Intelligence kwani hakuna jambo la hatari kama "self resentment". Hii inazidi kumjegea Rais Kagame Giza zito ndani ya Utu wake, a massive dark-side in his personality!

Kama unaimani kwa Mungu unaweza kutambua kuwa Huwezi kuwa karibu na Mungu au kuwa kwa Mungu wakati huo huo ukawa na full of negativity. Ikiwa na maana kuwa Mungu ndiye mjenzi mkubwa wa Strong Personal Emotional Intelligence.

Kama Kagame is full of negative emotions kwa sababu mbili kubwa, 1. Ombwe la Baba 2. Kutojikubali, Kujichukia yeye mwenyewe (Kama alivyosema AshaDii hapa Food For Thought | AshaDii ) na akingangania hali hizo, matokeoa yake ni kujiweka mbali na Uungu ambao uko ndani ya kila mwanadamu. Kwa watu wengine wanafikia kuwa completely disconnected na dhana nzima ya Mungu na thamani zake zote kama Utu, Ubinaadamu, Upendo nk. Anaweza kuwa katili, rebel nk!!!

Sitaki kuendelea kuhusu Ugonjwa wa Kagame ...! Cha Msingi ajue kuwa anatibika!!

Jambo la msingi sisi sote tugundue kuwa Hakutaka kuwa alivyo. Personally nampenda but not the energy which has made the home in him ... Na namshauri a let go all the dark forces of his past, (AJIFUNZE NA AWEZE KUSAMEHE KAMA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE WA TANZANIA ANAVYOMSHAURI) he will then rejuvenate internally and externally hata Mwili wake will be in a good shape amabyo amekuwa akiiota tangu utotoni! Isn't this what friend are for..? To give each other a reasonable and healthy advice?!!

Hakika najua atasoma hapa! Ni vema atambue kuwa the dark forces he is carrying arround his aura ... it is the one which is motivating him to terrorize the humanity arround the great lakes, something which isn't good at all!!

In real sense it is not him BUT something which has made home in him (The wrong emotions/energy) which we are addressing as a terrorist, a dictator, a sociopath and all the ill personality! WE STRONGLY ADVICE HIM NOT TO IDENTIFY WITH THE WRONG IDENTITY IN HIM ... by letting go through reconciliation and forgiving!!!
 
BekaNurdin,

Wewe mtu kama hii sio Kagame obsession lazima utakuwa mwendawazimu wewe,na lazima uwe mwehu kuandika ulichoandika,lakini FYI Kagame and Rwanda will never go back pre 94 na wote waliohusika na genocide justice wataipata hata after 100yrs
 
Kagame and Rwanda will never go back pre 94 na wote waliohusika na genocide justice wataipata hata after 100yrs
Justice for the genocide culprits ingeanzia kwa Kagame tungeamini unachosema kuwa kweli. Hata kama Kagame atakwepa justice yake hapa duniani kwa Mungu hataikwepa, ni heri angetubu uovu wake wote na damu ya Wanyarwanda aliyotoa kafara atasamehewa, atawekwa huru na atapata amani moyoni.
Kagame & Co. inaonesha mna tatizo kubwa sana kiroho, inafaa mfanyiwe deliverance kwa sababu mna demonic possession ndiyo maana mta-extend hate and vengeance to about 100 yrs hata kwa watu ambao hawakuhusika kwenye genocide. Kimsingi 40 yrs after genocide wahusika wote (including baba yako Kagame) watakuwa wamekufa iwe kwa kuuawa au hata natural death, sasa after 100 yrs mtawahukumu akina nani kama siyo kupagawa na mapepo ya kuzimu? Tatizo la Kagame ni la kiroho, akibadilika kiroho (spiritually transformed) his outward world will automatically change hapo ndipo Rwanda na Wanyarwanda watakuwa wamepona.
 
Azimiojipya umenimaliza kabisa. Kusoma madini kama haya kunafanya akili ya mtu inawiri kila siku. Am so thankful to have read this post.
 
Azimiojipya umenimaliza kabisa. Kusoma madini kama haya kunafanya akili ya mtu inawiri kila siku. Am so thankful to have read this post.

Ni muhimu serekali iwe na kitengo muhimu cha National Emotional Intelligence Unity kuweza kudeal na Watu kama Kagame kwenye kina cha Tatizo lake!! Huyu dogo hahitaji Physical combat ... Ku deal Naye!! Huhitaji kuwasiliana naye through time and space...!!
 
Back
Top Bottom