Ni kosa kujipa matumaini hewa. Kuna mambo yanahitaji gharama kubwa

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo wote!

1. Matumaini hewa ni kujidanganya

2. Kukwepa wajibu!

3. Kuukimbia ukweli.

4. Ukweli ni kuwa kuna mambo yanahitaji gharama kubwa ikiwezekana kulipia gharama ya uhai ikibidi ili kuyapata.

5. Maisha ni muhimu sana. Uhai ni zawadi ya mara mara moja. Lakini siku zote ukiogopa kufa kuna mambo hutoweza kuyapata Abadan.

6. Kufuata mkumbo ni pamoja na kutokuwa tayari kwa matokeo kwa kile unachokipigania. Hasa michezo hatari au kupigania jambo kubwa kama haki na uhuru.

7. Kama umwepesi wa kukata tamaa haushauriwi kuingia kwenye vita vya haki na uhuru.

8. Kama hauna stamina ni vizuri ukajipanga upya.

9. Kutegemea ushindi wa mezani hilo halitotokea kamwe kama unahitaji jambo kubwa kwenye maisha. Jambo kubwa huhitaji gharama kubwa. Sio ushindi wa kupewa.
Hayo yote ni muhimu watu wajulishwe mapema na wafundishwe ustahimilivu na moyo ujasiri.

10. Kutegemea nchi zingine zitoe msaada kwa jambo lako kubwa ni sawa na mtegemea cha nduguye hufa maskini.

11. NO ONE WILL SAVE US.

12. Mungu awabariki wote.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ndio leo unajua? Endeleeni tu kumtetea huyu mtu wenu.

Ni wazi uteuzi umekuacha na butwaa, ila ndio saaa mjifunze nyie wenye vichwa vigumu.
 
Uko sahihi sana taikuni
Bila mapambano ya nguvu na mipango madhubuti hakuna ushindi.

Nimejikumbusha hapa baada ya kusoma andiko lako
Mathayo 11:12 Ufalme hupatikana kwa nguv, nao wenye nguvu wauteka.

Hii ilikuwa muktadha ya Ufalme wa Mbinguni lakini ndio hivyo pia kwa falme za duniani

#SioRahisi #Inawezekana
 
Mwisho ushafika bado tu kidogo mambo yote yatakuwa sawa.

Mwanakondoo ameshinda tumfuate
 
9. Kutegemea ushindi wa mezani hilo halitotokea kamwe kama unahitaji jambo kubwa kwenye maisha. Jambo kubwa huhitaji gharama kubwa. Sio ushindi wa kupewa.
Hayo yote ni muhimu watu wajulishwe mapema na wafundishwe ustahimilivu na moyo ujasiri.
Hizi gharama bado Watanzania wengi hawapo tayari kuzibeba, bado wanaamini Ukombozi kwenye Taifa lao utaletwa na watu "fulani".

Hii "Gharama" ndio watawala wanaitumia mara zote kutishia watu, kwamba watakufa wataacha familia zao na majonzi.

Nashauri WAOGA wote wafunge midomo yao na waache majasiri walio tayari wafanye wanachoona kwao ni sahihi, Usaliti ni pale MUOGA unapomkatisha tamaa mwenye Ujasiri.
 
Naibu Waziri Wa Elimu....
😭😭😭😭

Ee Mungu...tunyooshee mkono wako watanganyika
 
Ogopa sana mtu anaepindisha ukweli na upo wazi kabisa
 
Mkuu kwenye ripoti yako ya zile vurugu kipande cha kimara,ulisema kuna njemba zilikuja kutia vibe zikitokea mbezi kuelekea kimara,hizo njemba zilikuaje,mtu za mazoezi au?..uliziona baadae?
 
Mkuu kwenye ripoti yako ya zile vurugu kipande cha kimara,ulisema kuna njemba zilikuja kutia vibe zikitokea mbezi kuelekea kimara,hizo njemba zilikuaje,mtu za mazoezi au?..uliziona baadae?

Ngoja nitaendelea maana. Bado afya yangu ya akili haijakaa vizuri
 
Ndio leo unajua? Endeleeni tu kumtetea huyu mtu wenu.

Ni wazi uteuzi umekuacha na butwaa, ila ndio saaa mjifunze nyie wenye vichwa vigumu.

Mtibeli siku zote anajulikana kwa Haki, kweli, akili na upendo. Ni hayo tuu Mkuu. Ushabiki hatunaga.
 
Huu upepo kitambo uje kutulia tutaona Mengi. It's gonna be a bumpy ride. So make sure you brace for impact
 
Amna kazi, serikali ya maza iko hovyo sana.

Nashindwa kuelewa ni kwanini anashindwa kuwawin wananchi aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…