Ni kosa kupakia picha za watoto mtandaoni.

Ni kosa kupakia picha za watoto mtandaoni.

magnifico

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
11,075
Reaction score
24,634
Juma hili tumepokea simu na hata
picha za simu katika Kituo cha
Huduma ya Simu kwa Mtoto zikiwa na
taarifa za kufanyiwa ukatili wa
kingono watoto wa kike.

Picha za watoto hao sasa zimesambaa
mitandaoni. Jambo hili linasikitisha
lakini baya zaidi ni usambazaji wa
picha hizi mitandaoni.

Kusambaza picha hizi ni kosa kisheria
na kama taasisi ya kuzuia ukatili kwa
watoto tunapinga vikali usambazaji
wa picha za watoto mitandaoni hasa
katika muktadha wa ukatili wa
kingono kwa kuwa kufanya hivyo
kunawadhalilisha watoto pamoja na
familia zao.

Mbali na hivyo hakuna ushahidi
uliothibitisha kuwa watoto wote walio
kwenye picha zinazosambazwa
wamefanyiwa ukatili huu na
kusambaza picha zinazoonyesha sura
zao iwe wameathirika au la
itawaathiri kwa namna moja ama
nyingine.

Vilevile, bado haijathibitika kwamba
ni kweli watoto wamefanyiwa kitendo
hicho na kila mtuhumiwa hata wa
ukatili kwa watoto anayo haki mpaka
pale itakapothibitishwa kuwa
ametenda kosa.

Tungependa jamii ijue kwamba kila
picha ama video yenye maudhui ya
unyanyasaji wa kingono kwa mtoto au
unyanyasaji wa aina yoyote
inapopakiwa, inaposambazwa au
inapotazamwa, mtoto huyo huathirika
na unyanyasaji huo upya.

Huyu ni mtoto alie hai na amepitia
ukatili wa kutosha. Watumiaji wa
mitandao nchini Tanzania wanaweza
kusaidia kulinda watoto walioathirika
na unyanyasaji wa kingono au ukatili
mwingine wanapokumbana nazo
mtandaoni na kutokuzisambaza zaidi.
Wengi wetu huona fahari kuwa wa
kwanza kupakia picha au video hizi
kwenye Whatsapp, Instagram,
Facebook na popote pale kwenye
mitandao ya kijamii bila kujua kuwa
hili ni kosa kisheria. Sheria mbili za
Tanzania zinatoa adhabu kwa makosa
namna hii.

Yaani Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009
ikisomwa pamoja na Sheria ya Makosa
ya Kimtandao mwaka 2015.
Sheria hizi zinatamka wazi kwamba ni
marufuku kupakia, au kuchapa picha
au video ya mtoto zinazohusu ukatili
awe hai au ameaga dunia. Kisaikolojia
binadamu wanajifunza vitu kwa kuiga
kile kinachogusa mihemko yao na
kukishuhudia kwa hiyo
hatuwafundishi watu kwa
kuwaonyesha video au picha zenye
maudhui ya kikatili bali
tunapozisambaza tunaendeleza ukatili
ilihali ulinzi wa mtoto ni jukumu letu
sote.

Ifike mahali jamii ifahamu kwamba
kila picha au video ya mwathirika
inapotazamwa, mtoto huyu hufanyiwa
ukatili upya kwa hiyo kabla
haujatuma picha au video ni vyema
kuwaza je ninamlinda huyu mtoto na
familia yake? Na je, jamii itajifunza
nini kwa kutazama picha hii?
Kumbuka, picha zina madhara kuliko
mafundisho. Tupo kwa ajili ya
kuwalinda watoto na sio kuwakatili
upya.

Tunaomba wale wote waliopakia
picha kuziondoa mara moja
mtandaoni na kutoendelea
kuzisambaza tena kwa maslahi ya
watoto pamoja na familia zao na kwa
maslahi ya watoto wote wa Kitanzania.
Jukumu la ulinzi wa mtoto ni letu
sote, tuwajibike.
Malezi ya watoto ni jambo la msingi
kwa ukuaji wa taifa letu. Tuwatunze.

Mwananchi 2020.
 
Kuna wale walimu huko shuleni wanamgeuza mtoto kama meme wanamrekodi mtoto wakimuuliza maswali na pasi na ruksa ya mzazi wanapost mtandaoni. Mtoto anageuka kituko.

Kuna siku atakuja kuchezea mtu vifuti vya pua hamtaamini.
 
Hahah wale ni watoto wakubwa.
Hahaha swadakta
Sahivi wazazi wanapost picha kuanzia kabla ya ujauzito, akiwa na ujauzito tena nusu uchi, siku ya kujifungua, mtoto ana siku 5 picha kibao, yaani mpaka anafikia ukubwani 18yrs online digital fingerprint yake ishakuwa kubwa na haki zake zishakiukwa sana inapelekea cyberbulling, kutapeliwa, na mambo kama hayo.
 
Hahaha swadakta
Sahivi wazazi wanapost picha kuanzia kabla ya ujauzito, akiwa na ujauzito tena nusu uchi, siku ya kujifungua, mtoto ana siku 5 picha kibao, yaani mpaka anafikia ukubwani 18yrs online digital fingerprint yake ishakuwa kubwa na haki zake zishakiukwa sana inapelekea cyberbulling, kutapeliwa, na mambo kama hayo.
Tatizo sana mkuu. Laiti wangekuwa wanajua madhara yake kwenye saikolojia ya mtoto huko mbeleni wasingekuwa wanafanya hivyo.
 
Back
Top Bottom