kuna kipengele katika muswada wa uundwaji wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya kwamba ni kosa la jinai kuhoji au kupinga au kukebehi maoni/maamuzi ya tume. Imekaaje hii?
kuna kipengele katika muswada wa uundwaji wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya kwamba ni kosa la jinai kuhoji au kupinga au kukebehi maoni/maamuzi ya tume. Imekaaje hii?
Nadhani tuanze kwanza kupinga muswada huo kabla hatujaendelea na mchakato wa kupata Katiba mpya. Hapo ndo naona lile swala la mtu kuogopa kivuli chake sasa anatafuta jinsi ya kukificha asikione!!!!!
Hivi mnategemea nini kumpa mamlaka fisi alinde butcher? Elewa kwamba baada ya kutokuwa na ruhusa ya kupinga matokeo ya kura za urais, sasa linakuja kwamba hakuna kuhoji tume ya katiba. Itakalosema, wadanganyika wote mseme kwa heruf kubwa "AMIN".
Kwa mwanzo huu, tegemeeni katiba inayokuja ndiyo itakuwa imelinda mambo mengi sana ya ovyo!.
MUNGU TUSAIDIE WATANZANIA WENGI TUSIOKUWA NA MTETEZI.