Lipi au yapi ni sahihi katika sentensi zifuatazo, naomba msaada kufahamu matumizi fasaha tafadhali.
--- Waziri ameapishwa na Rais
--- Waziri ameapizwa na Rais
--- Waziri atamwapisha katibu wake
--- Waziri atamwapiza katibu wake
Akhsanteni.
SteveD.
Kuapisha ni kumfanya mtu ale kiapo. Kuapiza ni kumtakia mtu mabaya.
Rais haapizi mawaziri bali anawaapisha. Kuna wazee wanaoapiza watoto wao kama hawawatendei haki.
Kwa nyongeza neno hapiza ni kumlani mtu...! Kuachiwa ladhi mbaya...
Yote sawa.
Hakuna haja ya complication SteveD
What is the root cause of that?