Ni kujiamini au ni uchawi? Wauaji walizurura na maiti kwenye gari hadi walipoamua kuitupa porini

Ni kujiamini au ni uchawi? Wauaji walizurura na maiti kwenye gari hadi walipoamua kuitupa porini

sepema

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2019
Posts
591
Reaction score
1,001
Heshima yenu wakuu. Miaka mingi nyuma mtu wangu wakaribu alinieleza kitu ambacho kiliniacha mdomo wazi.

Ni hivi, yeye nawenzake walitoka safari flani ambayo ilibidi wapande gari. Wakati wapo barabarani wakajaribu kusimamisha pickup flani ambayo ilikubali kuwachukua kwani walikua wanelekea uelekeo mmoja. Ndani ya gari hyo walikuepo watu wa3 akiwemo dereva na waliopewa msaada walikua wa4,wote wanawake.

Katikati ya safari mmoja kati yawaliopewa msaada akahisi kitu kisicho cha kawaida kwenye lifurushi lilokuwa hapo walipo,ikumbukwe Hawa waliwekwa Upande wanyuma wa gari.

Baada yakukonyezana na kudadisi wakagundua nimwili wabinadamu ambaye alishapoteza uhai(amekufa).

Kumbe wakati wakukonyezana wale jamaa kule mbele waligundua hivyo ghafla wakasimamisha gari nakuwarudia wale abiria wao. Wakawakoromea kuwa hawapaswi kushughulika na yaliyomo kwenye gari na endapo watakaidi nao watakutana na kilichompata huyo marehemu.

Wamama wale wakala kimya safari ikaendelea. Abiria wale walifika walipokua wanaenda ambapo gari Ile iliwashusha bila hata masharti yakutosema walichokiona.

Kama haitoshi,kwa kuwa sehemu hiyo ilikua imechangamka flani jamaa walipaki gari wakaingia bar kupata bia na nyama choma bila wasiwasi.

Kesho yake ikapatikana taarifa ya mwili wa mwanamke uliookotwa kwenye pori jirani na eneo waliloshukia wale akina mama.

Najiuliza, kwanini hawa watu hawakuogopa kukamatwa hata baada yawatu kugundua mwili kwenye gari yao?
 
Kwa sababu WaTz ni waoga, hatujui haki na wajibu wetu, hatujali yampatayo yeyote mpaka yatukute.
Wengine huyatumia yote haya kufanya watakavyo.
 
Hivi vitu huwa vipo.

Inasemekana ukipewa kazi ya kusogeza glass iliyolengwa ukafanikiwa na wewe lazima uhamishwe sayari, refer kisa cha yule mwenye degree tano na mdada wa taulo ofisini.

Refer pia mdada wa futari hoteli nyota tano kwa Mtambuzi

Dunia ina mengi ya ajabu ajabu
Unajua Maisha yanaumiza kichwa sana? Embu rahisisha basi hata kwenye hiki tuelewe
 
Hivi vitu huwa vipo.

Inasemekana ukipewa kazi ya kusogeza glass iliyolengwa ukafanikiwa na wewe lazima uhamishwe sayari, refer kisa cha yule mwenye degree tano na mdada wa taulo ofisini.

Refer pia mdada wa futari hoteli nyota tano kwa Mtambuzi

Dunia ina mengi ya ajabu ajabu
Kuna mambo mengi humu duniani hatuyajui na siku tukiyajua dunia itakuwa tofauti
 
Kwa sababu WaTz ni waoga, hatujui haki na wajibu wetu, hatujali yampatayo yeyote mpaka yatukute.
Wengine huyatumia yote haya kufanya watakavyo.
Well Said !!!!
 
Back
Top Bottom