Ni kulipa mahari au kutoa mahari?

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
73,773
Reaction score
102,126
Habari zenu wana MMU,

Binafsi nimekuwa nikichanganywa na hizi kauli mbili;

1. Kutoa mahari

2. Kulipa mahari

Je, ipi ni kauli sahihi?
==================




 

Attachments

  • mahari.jpeg
    34.1 KB · Views: 228
Ni kutoa mahari bwana, kwani unanunua gari hata iwe kulipa?
 
Yote mawili yako sawa tu inategemea unaenda kwene kabila gani, ila kwa watani zangu kule lazima iwe ni kulipa
 
Mkuu huu uzii ungeupeleka jukwa la lugha ungepata ufafanuzi wa kutosha.
 
Kutoa kishika uchumba..........................
 
zote sawa..lkn watu wengi wanatumia kutoa mahari maana ukisema kulipa ina maanisha mke wako mtajariwa yuko worth kulipiwa ng'ombe au mbuzi ndo umchukue...dont think so
 
Habari zenu wana MMU!
Binafsi nimekuwa nikichanganywa na hizi kauli mbili;
1. Kutoa mahari
2. Kulipa mahari

Je, ipi ni kauli sahihi?

Kutoa - huku ni kuhamisha umiliki wa kitu kwa kupenda ama kutopenda.

Kulipa- ni kutoa ila kuna ulazima kwenye kufanya hivyo...kimila ni lazima kutoa mahari, kama unamtaka binti wa mtu sharti utoe mahari.

Conclusion- binafsi naona tunalipa mahari kwa sababu ni lazima tufanye hivyo.
 
Ni kutoa mahari bwana, kwani unanunua gari hata iwe kulipa?
mmh neno "kulipia mahali" limekuwa likihusika pia MadameX...wanaume wengi huwa wanaorodheshewa mambo kibao, then huruhusiwa kubargain
 
Last edited by a moderator:

SO, mkuu ni kuwa mahari inalipwa na sio inatolewa?
 
Nakubaliana na wewe.
 
SO, mkuu ni kuwa mahari inalipwa na sio inatolewa?

Mkuu mahari hulipwa...

Hata ukimchukua mke na umelipa nusu hilo huwa deni na heshima yako ukweni inalegalega. So we have legal, cultural and moral obligation to pay. That is much more than 'simply kutoa'.

Binafsi sioni vibaya kulipa wala sioni shida kulipa. Na hatumnunui huyo mwali bali we pay kulinda heshima zetu.

Umuhimu

Hii ni kuonyesha appreciation, kwa sababu utamchukua mwali umpe jina lako la mwisho, aende akakae kwako na akuzalie watoto na aongeze jamii yenu.

Huwezi kumnunua mtu atakeyeweza kufanya yote hayo, those things are priceless! So wakwezo ni kama wamekulelea mke na wewe kwa sababu umempenda it means umeona kazi kubwa waliyoifanya na usingependa umchukue tu bila kuonesha umeona kazi waliyoifanya (aka asante).

Yaani inatakiwa hata kama hawataki mahari uwaombe wachukue (You have to appreciate the toil/work of others!)

Binafsi sikubaliani na harakati za kufuta mahari because we will be living in selfish world where no one appreciates others work simply because watu fulani walikosa maarifa na kuona ni kama wanamnunua mke na kuanza kumtesa.

Finaly, mi hata kama wakwe zangu hawataki mahari I have to give them something.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…