Mpap Ndabhit
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 331
- 416
Naongea na mheshimiwa Lukuvi uliyeongoza ujumbe mzito na wenye matumaini Kwa watu wa Ngorongoro. Dunia na watanzania Kwa ujumla walikuwa wanafuatilia Kila Neno ulilotamka Kwa jamii ya watu wa Ngorongoro.
Ulibeba ujumbe mzito wa Mheshimiwa Rais. Hata hivyo Nina wasiwasi na kazi nzuri uliyoifanya isije kuwa heshima Yako Kwa jamii ni ya kutumika vibaya. Na sijui kama kweli Rais alikutuma.
Uliwahi kuja Sae Mbeya kwenye mgogoro uliodumu Toka mwaka 1960 kati ya wananchi na chuo Cha kilimo uyole.
Kwa kauli Yako na ushahidi upo ukiambatana na spika Tulia, Mkuu WA mkoa wa in Mbeya ulisema umetumwa na Rais Samia kumaliza mgogoro huo. Ukawarudishia heka 67 wananchi. Watu wakafurahi, Wakashangilia serikali ya CCM! Wakaanza ujenzi mara Moja.
Ulipoondolewa cheo chako akaja JERRY SLAA waziri ardhibKwa kushirikiana na BASHE waziri wa kilimo wakamdanganya Rais, wakaanza kuwasimanga na kuwatesa wananchi, wakaleta jeshi kung'oa na Kuharibu mazao ya wananchi. Wakaamuru watu wabomoe nyumba na mpaka Leo eneo limezungushiwa ukuta wa mabilioni huku wananchi wakiwa ndani hawajui hatima. Wamefungua kesi mahakama Kuu Mbeya ambayo hata hivyo haiwezi kuwareshea eneo lao Kwa kuwa serikali ya Samia imewakamia kupora eneo lao!
Leo wananchi wanaitwa wavamizi na kauli ya LUKUVI Wanasema ilikuwa ni siasa tu Tena uhuni!
Sasa huko Ngorongoro walikokupeleka mheshimiwa huoni kama wanakudhalilisha tu.