dour
Member
- Aug 7, 2017
- 7
- 9
UTANGULIZI.
Maendeleo katika taifa yanaletwa na miundombinu ya uhakika nyanja zote za uzalishaji na usafirishaji. Serikali imekua ikitimiza miradi mikubwa ya kimaendeleo ambayo imekua ikitekelezwa kwa awamu. Utekelezwaji huu unahitaji ununuzi wa malighafi kwajili ya kukamilisha miradi hiyo. Eneo hili la ununuzi linahusisha upatikanaji wa bidhaa, kandarasi za ujenzi pamoja na huduma. Inakadiriwa serikali hutumia zaidi ya 70% ya bajeti yote katika manunuzi.
Eneo hili la manunuzi ya serikali linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinasababisha matumizi ya fedha za serikali yasiyokua na tija kwa taifa. Changamoto kubwa zilizo bainishwa na ripoti ya CAG ni ubovu wa mfumo wa ununuzi kua na mianya ya rushwa na ubadhilifu. Kupitia mamlaka ya ununuzi wa umma (PPRA) walianzisha mfumo wa kieletroniki uitwao Tanzania Natinal e-procurement system na badae kuboredhwa na kua NeST. Japo mfumo umeboreshwa napendekeza yafuatayo kuboreshwa katika huo mfumo wa kieletroniki ili kudhibiti mianya ya rushwa na ubadhilifu zaidi.
1. Mfumo uunganishwe moja kwa moja na ofisi ya CAG.
Ofisi ya CAG inayo dhamana kupitia na kukagua kazi zote za serikali pamoja na ununuzi, ili kuboresha ufuatiliaji katika ununuzi na utoaji zabuni kwa njia ya kieletroniki napendekeza mfumo huo wa NeST kuweza kuunganishwa na kusomana moja kwa moja na ofisi ya CAG. Ofisi hii ya CAG itapata nafasi ya ukaguzi kwa urahisi kieletroniki kufanya hivi kutaongeza uwazi na ukweli katika manunuzi ya serikali.
2. Mfumo kutumia akili mnemba kuchakata na kuchagua wazabuni.
Badala ya kuchakata na kuchagua wa wazabuni ambao hufanywa na watumishi wa serikali. Tungeboresha kipengele hichi kwa kuruhusu akili mnemba kulinganisha sifa zilizowekwa na sifa za wazabuni kisha kuchagua wazabuni. Akili mnemba itapunguza upendeleo na kuweka misingi ya haki katika utoaji wa zabuni. Hili litapunguza rushwa na kupata wazabuni wanao stahiki wenye sifa.
3.Mfumo uainishe bei za manunuzi kabla ya kutoa zabuni.
Moja katika sababu iliyotajwa na ripoti ya CAG ni kuongezwa kwa bei za bidhaa zinazonunuliwa na serikali, ukilinganisha na bei zilizopo sokoni. Hii inatokana na rushwa na usimamiaji wakusuasua, kudhibiti hili kila bidhaa ianishwe na gharama zake katika mfumo, wazabuni watakao ridhia bei ndio watakaopewa tenda. Kuwepo kwa bei elekezi kutapunguza rushwa na ubadhilifu katika ununuzi wa umma.
4. Kujumuishwa kwa kiswahili na lugha mbalimbali kwenye mfumo.
Mfumo wa NeST unao tumia lugha ya kingereza bado ni wakibaguzi hasa kwa wazabuni wenye sifa ambao bado hawajajua lugha hiyo. Hii inaleta upendeleo kwa wazabuni wa chache na kufanya maombi ya zabuni kuwa si ya haki. Napendekeza kujumuishwa kwa lungha ya kiswahili ili kuweza kuleta usawa wa kilugha na kitoa fursa kwa wazabuni wa ndani wenye uwezo kupata nafasi.
5. Mfumo kusomana na mifumo mingine kwa urahisi.
Mifumo ambayo inapaswa kusomana na mfumo huu ni pamoja na TRA, TAKUKURU, na ofisi ya mkurugenzi. Malipo yote ya manunuzi yanahitaji kuwa na risiti ili kusaidia taarifa za miamala, mfumo unatakiwa kusomana na TRA moja kwa moja. Ikiwa kutabainika ishara za rushwa basi mfumo utoe nafasi kuwasilisha malalamiko moja kwa moja TAKUKURU kupitia mfumo. Mkurugenza anajukumu la kukagua manunuzi na kuwasilisha ripoti ya mrejesho, hivyo mfumo unapaswa kua na sehemu ya mrejesho wa mkurugezi katika ufuatilaji.
6.Utangazwaji wa zabuni pamoja na fedha elekezi za miradi kieletroniki.
Miradi yote ya serikali inatakiwa itangazwe na kuwekwa wazi si tu kwenye mfumo bali ata mitandao ya kijamii. Wasiishie tu kutangaza tenda lakini pia watangaze fedha zote zilizo elekezwa kwenye miradi. Hii itaongeza uwazi na ugumu katika wizi wa fedha za umma.
Badala ya kupokea meseji za kubeti kwenye simu zetu sasa tunaweza kupokea meseji za zabuni pamoja na meseji za fedha elekezi za miradi inayopatikana kwenye jamii zetu. Uwazi huu utarahisisha ufuatiliaji wa miradi si kwa wakaguzi tu lakini hata wananchi wote kwa ujumla.
7. Mfumo uweze kuwalipa moja kwa moja wazabuni bila kupitia kwa wasimamizi.
Kumekua na mjadala mkubwa juu ya
wazabuni waliopewa tenda lakini hawakulipwa na hatimae kufilisika. Badala ya malipo kupitia kwa wakurugenzi kisha wakurugenzi kuwalipa wazabuni, kunayo haja ya kuwalipa wazabuni moja kwa moja kupitia mfumo baada ya mkurugenzi kuwasilisha ripoti ya tathimini. Kufanya hivi kutapunguza rushwa kwa kiasi kikubwa.
8. Kutumia teknolojia ya blockchain katika mfumo.
Katika ripoti ya CAG kumekua na malalamiko ya kufoji taarifa za manunuzi, pamoja na kufoji miamala ambayo pia inatumia namba ya malipo. Blockchain ni mfumo unaoweza kudhibiti ubadilishwaji wa taarifa kwa yeyote katika mfumo. Kwa kutumia teknolojia hii ya blockchain itasaidia kwa asilimia kubwa wa halifu wa kimtandao katika kubadili taarifa katika mfumo. Hii itasaidia kabisa katika usalama wa mtandao na kuzuia ulaghai.
9. Kuongeza kasi ya mfumo na mchakato wa kutoa zabuni katika mfumo.
Kuongezwa kwa wataalamu wa kuchakata data pamoja na kasi ya mfumo kuchakata data kwa muda mfupi utasaidia miradi ya serikali kutimia kwa wakati bila kuchelewa. Mfumo unatakiwa uendane na teknojojia mpya hivyo ufanyiwe maboresho kila wakati.
HITIMISHO.
Kwa ujumla maboresho hayo ya mfumo wa kieletroniki katika manunuzi unapaswa kwenda sambamba na maboresho ya sera za ununuzi wa umma. Mamlaka husika za ununuzi wa umma zinalojukumu katika kuwaelimisha wananchi wote juu ya ununuzi wa umma. Kuboresha mifumo hakutoshi endapo mamlaka husika hazitatoa adhabu kw wabadhilifu hivyo nashauri serikali kua na adhabu kali kwa wabadhilifu wa mali ya umma.

Upvote
4