Ni kwa nini miss judy?

Sabalkheri Waungwana; habari na tupashane;
Leo Tumeonana; mjadala na ufane
Mjadala wenye maana; sote tushirikiane;
Kwangu Miss au Mama; Ni kama manemane . . .

Duh! Nimepotea njia. Kwa kheri.

Was nice reading here. very fun.
 
Ha ha ha...kweli kipaji unacho...hongera sana miss Judy oopss mlimbwende Judy, nimekubali kweli ww ni mlimbwende na sio miss
 
ha ha ha, kweli huku JF kuna watu wenye vipaji....excellent job
 

Dada Judi we hongera, umejibu kwa hekima
washikilia bikira, ulivyofunzwa na mama
wachache wenye subira, kisha wanalia "mama"
jitunze na kujijali, Atakupa kama wewe!
 
Nyote niwategaji.
Mishipi ndani ya maji.
Miss J na na muulizaji.
Mwajaribu kupima maji.

Nyote mwavinjali
Miss Judy na Rijali.
Munaanza na maswali.
mwisho mwavua suluali.

Hapo hakuna mwali
hapo hakuna rijali.
mwaeleza zenu siri.
mwatafuta yafahari.

peaneni namba ifichuke siri.
kutaneni tujue yupi mkweli
Sisi siwazungu ni waswahili.
Tumeshaelewa yenu mashairi.

Musisahau mwevuli.
Muendako mbali.
Muvalishane vizuri.
musijepata homa kali.

Mimi si mshairi,bali msema kweli.
Maneno simsumari,kamanimekosa nitakiri.
Munisamehe washairi,Miss J na Rijali.
Musinione dalali,nilitaka toa tu tahadhari.
 
uwiiiiii
mie nilikua wapi,kuona hizi tenzi,
nahangaika na kwingine,ilhali hapa bayana,
kweli fani ni yetu halisi,kuenzi zetu tungo,
kweli nimewachwa hoi,watu kumendea vya watu.

kwanini umendee vya watu,hadharani kujimwaga,
kama kweli u-rijali mnona waonyesha woga,
kuiita kadamnasi,hapa jf kujieleza,
hizo ni dalili za woga,pasi kwenda pm.

kwanini hujenda pm,mlimbwebde kumsabahi,
ni jambo lililo la kheri,siri yako kuhiifadhi,
sema nae kwa sirini,labda utaipata yako tunu,
Kashaija ulifikiri nini,mlimbwende haanikwi.

mlimbwende haanikwi,hadharani kama mahindi,
mafunzo ya mama yakini,ya sirini ndio majibu,
rijari hufata nyumbani,wazazi wake kujitosa,
ongoza lako guu,upate lake kwa heri...

ha ha ha nilikuwa wapi siku zote hizi???
 

mpendwa msemakweli, karibu useme kweli,
mwambie huyo rijali, ajue nani tapeli,
kama aitaka mali, asiwacheze mafahali,
hatumtaki fedhuli, tunauenzi ukweli.

huyo rijali yu doro, ataka pa kuhemea,
nimemuweka kiporo, apate pa kusemea,
ausetiri uharo, huo umemlemea,
hatumtaki fedhuli, tunauenzi ukweli.

kashaija alikuja, butege nilimtega,
hakufanikiwa paja, urijali ulimtega,
niliogopa viroja, ni wengi aliwamwaga,
hatumtaki fedhuli, tunauenzi ukweli.

iweje huoni mwali, upofu watakiani?
kama ungekuwa wali, tungetiana shakani,
heri ya hiyo asali, tamu tumeibaini,
hatumtaki fedhuli, tunauenzi ukweli.

namba sitaihitaji, mie ninae wangu,
yeye pekee mtaji, kwangu amekuwa rungu,
hakuna tena ujuaji, katukutanisha Mungu,
hatumtaki fedhuli, tunauenzi ukweli.
 

hata aposti piemu, hesabu kaikosea,
yupo aliyehitimu, tayari kanipokea,
asilaumu walimu, shauri kulikosea,
bikira mali adimu, masikini kakondea!

iwapo kandamnasini, yamchoma nafsini,
kajichokea windoni, na ramani kasahau,
yapasa kuadhini, na mistari kuighani,
bikira mali adimu, masikini kakondea!
 
Hongereni waungwana karibu mtapatana
Nimesoma na nanena kuwaombea bayana
Mtamjua tu sana bila hata kulumbana
Waji na yake tabia kuhusu huyu bi Judy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…