Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
nimekusoma nshairi, nao wako udadisi,
utata umeukiri, mzito na si mwepesi,
kujibu bila kiburi, jibu linaloakisi,
si sawa kuita kiti, sahihi ni kitumoto
kiti kikiwa moto nani atakalia,
iwe mrisho mpoto, mie na wewe sawia,
ikiwa ni kitumoto, na joto lote twabwia,
si sawa kuita kiti, sahihi ni kitumoto
nimekusoma nshairi, nao wako udadisi,
utata umeukiri, mzito na si mwepesi,
kujibu bila kiburi, jibu linaloakisi,
si sawa kuita kiti, sahihi ni kitumoto
kiti kikiwa moto nani atakalia,
iwe mrisho mpoto, mie na wewe sawia,
ikiwa ni kitumoto, na joto lote twabwia,
si sawa kuita kiti, sahihi ni kitumoto
Hapa mie nakujuza, kitimoto maana yake,
Ulapo nakueleza, lazima na moto wake,
Utamu wake wakaza, kikiwa na moto wake,
Hili ndilo jibu lake, kwa swali lako sikia.
Asili yake ni bongo,likaenda nako Kenya
Uganda wao si bongo, kitimoto kutopenya,
Jina hili si uongo, ni la mpito kupenya,
Hili ndilo jibu lake, kwa swali lako sikia.
Jina limejizolea, umarufu Tanzania,
Umakini elezea, wahitajika sikia,
Yasiwe ni mazoea, unene kuwaingia
Hili ndilo jibu lake, kwa swali lako sikia.
Kiti moto asili yake ni kipindi cha tv,cha dtv kilikuwa kinaendeshwa na pascal mayala...kilikuwa kinaitwa kiti moto....
Kiti moto asili yake ni kipindi cha tv,cha dtv kilikuwa kinaendeshwa na pascal mayala...kilikuwa kinaitwa kiti moto....
Soma mwenyewe! Hajawalaana aliwatumia kumponya mgonjwa. Kwa bahati mbaya au nzuri walikuwa karibu na uponyaji huo.Enyi walaji wa kitumoto ama kitimoto sijuwi naomba msome kitabu cha biblia injili ya marco mtakuta yesu alimlaani nguruwe!!
Nyama tamu kupita zote duniani.na mshindwe na mlegee ninyi mnaonikumbusha kitimoto....mnanifanya niache shughuli a kujenga taifa letu tukufu nikamtafute alipo......mshindwe tena mshindwe....huyo huwa hatajwi mida ya kazi jamani...nasema mshindwe...hata JF nita-SIGN OUT....kwa sababu ya mwanzisha mada....nimesema mshindwe katika ujenzi na uendelezaji wa taifa hili asitajwe popote pale kwani atarudisha nyuma maendeleo....!
ANGALIZO; WAISLAMU,WASABATO & CO.......MSIJE MKALOGWA MKAJARIBU HIYO KITU IACHANE KABISA ILI WALAJI TUZIDI KUWA WACHACHE
OMBI; MNISAMEHE KWA KUTOKUJIBU SWALI....ILA MAELEZO YANAJITOSHELEZA
Salam kwako Kashaija, Judi nawe Achengula
Nami ulingoni naja, kitimoto nami nala,
Nauvutiwa lake paja, maini nayo salala,
'Kitumoto' masihala, 'Kitimoto' muhamala.
Achengula amenena, asili yake ni bongo
Kitimoto hata China ,utaikuta si uongo
Sinza Afrika Sana, watu wala kwa usongo,
'Kitumoto' ni uongo, 'kitimoto' ndilo jina.
Juzi nilikula kona, na bibie nyumba ndogo
Starehe niloona, nisingeipa kisogo,
Ikaletwa iliyonona, na kachumbari ya tango,
'Kitumoto' ni uongo, 'kitimoto' ndilo jina.
Judi hapa nakupinga, ''kitumoto' si nguruwe,
Hili lako umetunga, kutoka kwenu Msewe,
Karibu kwetu Ukonga, kilo moja ufungiwe,
'Kitimoto' ndo nguruwe, 'kitumoto' nakupinga.
Kiti moto asili yake ni kipindi cha tv,cha dtv kilikuwa kinaendeshwa na pascal mayala...kilikuwa kinaitwa kiti moto....
Enyi walaji wa kitumoto ama kitimoto sijuwi naomba msome kitabu cha biblia injili ya marco mtakuta yesu alimlaani nguruwe!!
Enyi walaji wa kitumoto ama kitimoto sijuwi naomba msome kitabu cha biblia injili ya marco mtakuta yesu alimlaani nguruwe!!
Nijuze wenye miito, ukweli nami nijuwe,
Nahaha kama mtoto, ninaranda kama mwewe,
Kichwa kinawaka moto, nimejawa na kiwewe,
Nijuze kwani nguruwe, anaitwa kiti moto?
Ewe malenga Mpoto, kihabarishe kijiwe,
Hivi ni neno mpito, mjuzi nani mwanzowe?
Nguruwe hata mtoto, kitimoto tambuliwe,
Nijuze kwani ngurue, anaitwa kiti moto?