Mkuu kuna mambo mawili hapa. Idara fulani inaweza kukutaka ubaki kuwa tutorial assistant mara tu baada ya kumaliza bachelor yako. Na hii ina maana kuwa umepasua kweli hasahasa ukiwa umepata first class au upper second ya nguvu. Pili kuna ku-apply mwenyewe pale chuo husika kinapotangaza nafasi za kazi za tutoria assistant (bachelor holder), assistant lecturer (masters holder) na lecturer (PhD holder).
Kwa walimu wa vyuo vikuu wanatumia scales za "PUTS" ambazo kwa PhD holder kwa sasa wanaanzia milion 3 na kidogo kwa masters holder ni around 2 mil na kwa bachelor holder ni milioni na kidogo. Wenye data kamili wanaweza kutupatia hapa