Ni kwanini gari za Singapore zinaogopwa?

Ni kwanini gari za Singapore zinaogopwa?

Franklee

Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
22
Reaction score
14
Cha kwanza inabidi ujue kuwa kumiliki gari ukiwa Singapore ni mtiti, kukamilisha usajili wa gari ukiwa Singapore inawezekana ikawa ni gharama zaidi hata ya Tz japo sisi tunatumia second hand wao hata mpya zinakua na gharama sana.



Kuna kitu kinaitwa Certificate of Entitlement (COE) hapa unapewa cerificate ya kumiliki gari miaka 10 tu, baada ya hapo inabidi u renew tena cerificate hii, inaweza kua 4x ya bei ya gari yaani gari ya mil 3 ukachajiwa mil 12 kupata hii certificate, imagine ukinunua gari ya mil 100 utalipia hii certificate almost mil 350+



Hapo weka mbali Additional Registration Fee (ARF) ambayo nitaita kama ushuru maana inaendana na ya huku kwetu. ushuru (ARF) ambao ni lazima utaanzia asilimia 100% (yaani gari ya mil 3 utalipa mil 3 au zaidi kulingana na vigezo vyao), na sometimes unafika hadi 180% (approximately mil 5.8) kwa gari ile ya mil 3, kuna gharama nyingi sana hapo kama vile registration fee, Vehicular emission scheme etc.



Mtego upo hapa kwenye additional registration fee



  1. Ukisema uachane na hiyo gari baada ya kutumia 5 years utarudishiwa 75% ya ile ARF ulilipa wakati unafanya registration (yaani kama ulilipa ARF mil 10 basi utarudishiwa mil 7 na laki 5)
  2. Ukitumia mika sita 6 inapungua taratibu utarudishiwa 70% na kuendelea kadri mika inavyoongezeka basi ndivyo utalipwa kidogo ile ARF yako.
  3. Gari ikiwa na miaka 9 utarudishiwa 50% yaani ile gari ulinunua kwa mil 100 ukalipa ARF mil 10 basi utapewa mil 5 kama de-registration refund
  4. Sasa gari ikitimiza 10years net hupewi kitu chochote zaidi zaidi ukifanya registration upya utapewa penalties za juu sana, ushuru utapandishwa, utalipa gharama za juu za emission nk


Kiufupi jamaa wanajua kabisa kumiliki gari zaidi ya miaka 10 kwao ni msala kwahyo mostly watatumia miaka michache bila kufanya major service kwasababu wanajua fika there’s no need ya kuingia cost zingine wakati wataachana na hilo gari ndomana they don’t care na magari yao mengi sana yanakuja history mbaya sana ya service ukilinganisha na gari zinazotoka stock location ya Japan na nchi nyingine.



Hali ya hewa ni joto sana na kuna foleni sana so engine zinakua zinapiga load sana ni kama gari za dar zinavyo washa AC full time, na pia kuna humid climate which affects the body kupelekea kutu etc



Singapore ni nchi ndogo wameweka vigezo vikali kuregulate traffic jams.



In conclusion magari yao ni unyama sana mostly ni top trim, na toyota ndo anaongoza kuwauzia magari akifatiwa na benz, toyota ya singapore hamna hamna utakuta 260kph kwenye dashboard, leather seats, sunroof etc.



Hakikisha gari unayochagua ni latest kwa maana ya kwamba ina miaka michache kule kwao au sijui kama una mtu akukagulie huko huko sijui kwakweli ila gari nzuri zipo na mbovu zipo nyingi zaidi kutoka Singapore.



Hakikisha unaponunua gari kutoka kwenye website unaangalia stock location ili ujiridhishe vizuri na kuongeza kujiandaa kulipokea gari lako.
 
Kuna gari nilikua naitafuta ya mwaka 2014 karibu zote nilizoziona bf na sbt zinatoka Singapore which means zimetimiza 10 years wanazisukumia huku Africa na hapo unakuta hakuna major service yoyote imewahi kufanywa
Katika maisha yako usinunue gari toka Singapore, nilinunua BMW kupitia SBT, najuta najuta najuta
 
Yani wananunua kutumia tu hakuna service wanahisi atakae nunua atafaidi sana, kuna moja tulikuta haina bearing moja kwenye drive shaft yaani it’s weird walikua wanafanya nini mpaka wakaitoa
 
Back
Top Bottom