Ni kwanini gundi (glue) haikamati pakiti yake?

M.J

Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
27
Reaction score
3
Jaman naomba kujuzwa kuhusu gundi zenye nguvu na zinazonasa haraka (powerful and fast glue) kama superglue miongoni mwa materials zilizoainishwa kuwa inaweza kunasa ni pamoja na zilizounda pakiti yake.

Ni kwanini haifanyi kazi hiyo inapokuwa ndani ya pakiti.
 
Nnachojua gundi inahitaj hewa ili igande na ndan ya pakti kunakuwa hakuna hewa ndomana haigand ila ukiifungua na kuruhusu hewa kuingia itaganda tuu.

Mkuu umejibu kisayansi. Naomba hii thread isiendelee kuja na majibu. Jibu limejitosheleza sawia
 
Nnachojua gundi inahitaj hewa ili igande na ndan ya pakti kunakuwa hakuna hewa ndomana haigand ila ukiifungua na kuruhusu hewa kuingia itaganda tuu.
mhhh kuna utata na gundi ya karatasi je mbona ukiitoa kwenye karatasi yake inatoka vizuri ila kwenye karatasi nyingine inakamata sawia
 
Jaman naomba kujuzwa kuhusu gundi zenye nguvu na zinazonasa haraka (powerful and fast glue) kama superglue miongoni mwa materials zilizoainishwa kuwa inaweza kunasa ni pamoja na zilizounda pakiti yake.

Ni kwanini haifanyi kazi hiyo inapokuwa ndani ya pakiti.
We jamaa umenifanya nijifikilishe vitu ambavyo sikuwahi kujishugulisha kuvijua
 
Mmezungumzia habari ya gundi. Japo inawezekana isiwe mahali pake. Mjomba wangu ameweka madirisha ya Aluminium na kwenye yale madirisha kuna zile nailoni za njano zimegandamana. Huu ni mwaka wa tatu sasa amejaribu kila njiani imeshindikana kuzitoa.
Anasema aliambiwa azitoe baada ya kupiga rangi nyumba. Amejaribu kwa mafundi wengi lakini wamemuambia ameshachelewa kwasababu zimeshachomwa jua na maji ya mvua hivyo gundi imekwisha.

Kwa yeyote mwenye uzoefu tatizo wa tatizo kama hili atusaidie ushauri
 
Cha msingi atoe anunue mengine alafu awahi kuondoa hizo karatasi othewise apotezee kama ni zaidi ya miaka mitatu kwani zina ubaya gani anatangaza biashara akachukue hela
 
atumie mafuta ya taa
 
Cha msingi atoe anunue mengine alafu awahi kuondoa hizo karatasi othewise apotezee kama ni zaidi ya miaka mitatu kwani zina ubaya gani anatangaza biashara akachukue hela

Majitu mengine kama waliokotwa chooni..
 
Mmezungumzia habari ya gundi. Japo inawezekana isiwe mahali pake. Mjomba wangu ameweka madirisha ya Aluminium na kwenye yale madirisha kuna zile nailoni za njano zimegandamana. Huu ni mwaka wa tatu sasa amejaribu kila njiani imeshindikana kuzitoa.
Anasema aliambiwa azitoe baada ya kupiga rangi nyumba. Amejaribu kwa mafundi wengi lakini wamemuambia ameshachelewa kwasababu zimeshachomwa jua na maji ya mvua hivyo gundi imekwisha.

Kwa yeyote mwenye uzoefu tatizo wa tatizo kama hili atusaidie ushauri

Ajaribu kutumia hair hand drier. Una connect kwa umeme hiyo hand drier, tumia joto itokayo ktk hand drier kupasha joto hizo nailoni na wakati huo huo uwe unabandua hizo nailoni.
 
We jamaa umenifanya nijifikilishe vitu ambavyo sikuwahi kujishugulisha kuvijua

Kweli kabisa, kina maswali mengine ya kitoto ila mpaka mtu ayafikirie, ni great thinker maana wengine tunayapuuza na kuishia kuishi bila kujua sababu zake.
 
Kwa upande wangu naona ni kwa sababu kunakuwa hakuna hewa ambayo inaingia kwenye chupa na ili gundi igande inahitaji hewa kwanza
 
Nnachojua gundi inahitaj hewa ili igande na ndan ya pakti kunakuwa hakuna hewa ndomana haigand ila ukiifungua na kuruhusu hewa kuingia itaganda tuu.

mkuu,gundi kamwe haiitaji hewa(oxygen)ili igande ...ukweli ni kwamba superglue imeeundwa na kemikali zinazoitwa "cyanocrylate",pindi hizi kemikali zinapokutana na majimaji hata kiasi kidogo cha unyevunyevu uliopo katika kidole chako au kwenye kitu chochote kile basi kemikali hizi zinaganda kwa haraka sana,sababu nyingine ya gundi kuganda nje ya pakiti yake ni hii;hewa pia inabeba kiasi kidogo cha unyevunyevu(humid)unao sababisha gundi kuganda punde tu inapotolewa nje..kwa maana hiyo basi gundi haiwezi kuganda ndani ya pakiti yake kwasababu hakuna majimaji au unyevunyevu wa aina yoyote ile, na wala sio ukosefu wa oxygen!
 
Back
Top Bottom