Ni kwanini Mahakama za mwanzo hawapokei ushahidi wa Kieletroniki?

Ni kwanini Mahakama za mwanzo hawapokei ushahidi wa Kieletroniki?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Wakuu,
Kuna Uzi fulani humu ndani umeanzishwa na wafanyakazi wa Mgahawa fulani Dar wakielezea uonevu waliofanyiwa na wamiliki wao ambao ni waarabu ikiwepo vipigo.

Sasa baada ya wao kupigwa na kugeuziwa kibao kwamba ndio walioleta vurugu,walipopoelekwa mahakamani kumbe walikuwa na ushahidi rekodi za CCTV au simu sikumbuki vizuri ila ushahidi ule ulikataliwa na mahakama ya mwanzo kwa kigezo kwamba mahakama hizo hazipokei ushahidi wa kielektroniki.

Sasa wataamu mtusaidie ni kwanini Mahakama za mwanzo hazipokei ushahidi wa namna hio?

Je hatuoni kwamba ni muda muafaka wa Ushahidi wa kielektroniki kuanza kupokelewa ili kuharakisha hukumu hasa ikizingatiwa kwamba matumizi ya simu,kamera na vifaa vingine vya sauti yanaongezeka na kuwa ya kawaida na hivyo kuturahisishia mambo?mfano mtu katukana na amerekodiwa mahakama ikaonyeshwa video si uthibitisho tosha huo?

Karibuni kwa ufafanuzi.
 
Wanasheria mmeenda wapi?
 
Back
Top Bottom