Ni kwanini ujenzi mkubwa au miradi mikubwa wanapewa wageni sio wazawa?

Ni kwanini ujenzi mkubwa au miradi mikubwa wanapewa wageni sio wazawa?

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
5,771
Reaction score
14,732
Ili jambo lina nishangaza sana au sijui elimu yetu inaonyesha kuwa na ukomo wa ushindani.Miradi mikubwa au ujenzi mkubwa sijawai kuona mzawa kashinda tenda au kufikirika mfano barabara kubwa,madaraja makubwa,magorofa marefu,viwanja vya mpira na n.k

Ni kweli kwamba sisi ujuzi wetu ni wanyumba za mapaa ya msukuma na barabara za mitaa
 
Ulimbukeni wa mtu mweusi hasa Mtanzania.

Wageni(Wachina) wanatoa Rushwa ambazo maofisa wa Serikali hawawezi kuzikataa.
 
Mkuu kama umewahi kufanya kazi na wakandarasi wetu wazawa utaelewa ni kwa nini wanapewa wageni na mimi nasema waendelee tu kupewa wageni kuepusha maafa.

Hivi unajua makampuni mengi hapa kwetu hayamilikiwi na wataalamu yaani ni yawanasiasa na wafanya biashara ambapo wapo after profit. Ukifanya nao kazi hawa watu wao ndio wanataka wakuelekeze mtaalamu namna ya kuweka ratio ya cement au ni material gani utumie kufanyia kazi sasa ukiwaeleza kanuni na taratibu za kazi wao wanahisi unataka wahujumu wanakufukuza kazi.
 
Ili jambo lina nishangaza sana au sijui elimu yetu inaonyesha kuwa na ukomo wa ushindani.Miradi mikubwa au ujenzi mkubwa sijawai kuona mzawa kashinda tenda au kufikirika mfano barabara kubwa,madaraja makubwa,magorofa marefu,viwanja vya mpira na n.k

Ni kweli kwamba sisi ujuzi wetu ni wanyumba za mapaa ya msukuma na barabara za mitaa
Wazawa kwanza wanapaswa kuacha uabbaishaji
 
Kuna ka lami hapa moshono ka kilometa moja ila wakuu walikajenga miaka miwili, mbaya zaidi waliaribu kabsa na miundo mbinu ya maji... wengine wamepewa kujenga road ya Sansi hapa jua likiwaka kali lami inayeyuka..
Kwahyo acha tu wachina wapewe kazi.
 
Sio rahisi kwa ufupi hawathibitishi ubora wao hasa wanapopewa kandarasi.
 
Wazawa wabishi sana kama unamwambia mtu amimine zege la nchi 5 yy anamimina la nchi 3. Unamwambia ratio ya plasta kwa mfuko ni vitoto ndoo 18 yeye anaweka 30. Unamwambia ukipanga jiwe weka mota yeye anaweka udongo, yaani ilimradi bundesliga. Wanawaza sana faida kubwa. Anataka kazi ya miezi 6 aifanye hata mwezi mzima ilimradi akunje faida nyingi.
 
Wakandarasi wazawa bado hawana vifaa vya ujenzi wanaokoteza vikukuu tu. Kulipa wafanya kazi na vibarua ni shughuli pevu hela hawana. Ujenzi hawajui wanakandika hovyohovyo tu. Ngoja wajifunze kwa wachina, wajapan na waturuki huenda wakaelewa
 
Ukiachilia mbali ufundi, mtaji ndio kinachowaangusha wakandarasi wa ndani kupewa kazi kubwa.
 
Iko hivi, Wewe unataka kujenga mradi wa Milioni 150 lakini mfukoni huna hiyo pesa, ila unataka kujenga nyumba kwa miaka 3, lakini utakuwa unalipa kidogo kidogo hadi nyumba ya milioni 150 ikamilike, sasa katika mradi wako kuna fundi ambaye anaweza kujenga kwa Pesa yake labda akatumia milioni 30 yake afu mkakubaliana wewe utamlipa baadaye yeye afanye kazi, afu kuna fundi yeye hana chochote anasubiri ukusanye milioni 30 umpe ndo aingie site, Ukiwa mwenye mradi utamchagua nani? Basi ndo kinachotokea kwa Miradi yetu mikubwa. Kikwazo kikubwa ni Ukosefu wa Mitaji ya kuendesha shughuli za miradi hiyo. Tunatamani kufika walipofika wenzetu lakini kukua ni Hatua, Uwezo wa Wakandarasi wa sasa na Miaka 30 iliyopita kuna tofauti kubwa, ukuaji upo. Na miaka 20 au 30 ijayo yawezekana hii miradi ikawa inafanywa na wazawa kabisa. Ukuaji ni hatua, hata wenzetu hawakufika hapo ndani ya usiku mmoja
 
Wazawa walio wengi kwanza hawajiamini.
Pili wakipewa fedha za mradi wanakimbilia kwanza kununua magari ya kifahari badala ya kununua nyenzo za mradi.
3.Miradi mingine upewa kama sehemu ya kuficha maovu ya wakubwa,miradi hewa.Inawaharibia CV.
4.Matumizi mabaya ya fedha yanasababisha poor finishing.
5.Poor estimate ya gharama ya mradi,mara nyingi ndio wanao tender kwa bei ya chini ambayo haiwezi kukidhi viwango.
 
Ili jambo lina nishangaza sana au sijui elimu yetu inaonyesha kuwa na ukomo wa ushindani.Miradi mikubwa au ujenzi mkubwa sijawai kuona mzawa kashinda tenda au kufikirika mfano barabara kubwa,madaraja makubwa,magorofa marefu,viwanja vya mpira na n.k

Ni kweli kwamba sisi ujuzi wetu ni wanyumba za mapaa ya msukuma na barabara za mitaa
moja ni uzoefu kazini, pili ni mtaji unaohitajika kwa ajili ya kufanyia kazi, mfano kupata mkopo benki ili aweze kufanya hiyo kazi (fedha kwa ajili ya kukodi zile mashine nzito za kufanyia kazi). Wachina wao tayari kampuni zimeshajijenga kwa hivyo wakipata tenda wanahamisha mashine kutoka saiti moja kwenda nyingine kwa gharama nafuu sana.

Jengine ni kuwa nchi yetu inachewelesha sana malipo kwa makampuni husika, kama unakumbuka hata hao wajenzi wa SGR and JNHPPP kuna kipindi walikuwa wanatishia kuhama kabisa. Sasa kivumbi kinakuja ikiwa kampuni ni ndogo na benki wanadai chao plus interest, mara unakuta jamaa amefilisika kutokana na madeni.

Pia changanya na asilimia ya rushwa inayodaiwa na hao wenye kupitisha hizo tenda, hilo nalo linadhoofisha utendaji wa kazi.
 
Wazawa walio wengi kwanza hawajiamini.
Pili wakipewa fedha za mradi wanakimbilia kwanza kununua magari ya kifahari badala ya kununua nyenzo za mradi.
3.Miradi mingine upewa kama sehemu ya kuficha maovu ya wakubwa,miradi hewa.Inawaharibia CV.
4.Matumizi mabaya ya fedha yanasababisha poor finishing.
5.Poor estimate ya gharama ya mradi,mara nyingi ndio wanao tender kwa bei ya chini ambayo haiwezi kukidhi viwango.
naunga mkono ili. mfano wachimbaji wa madini yani kapata milioni 900 za dhahabu baada ya kuboresha mgodi anaenda kitambaa cheupe kumaliza milioni 12 kwenye mishumaa na bango
 
1.mitaji
2.wataalamu Jina yani siyo wataalamu
3. wizi
4. kazi mbovu
 
Ili jambo lina nishangaza sana au sijui elimu yetu inaonyesha kuwa na ukomo wa ushindani.Miradi mikubwa au ujenzi mkubwa sijawai kuona mzawa kashinda tenda au kufikirika mfano barabara kubwa,madaraja makubwa,magorofa marefu,viwanja vya mpira na n.k

Ni kweli kwamba sisi ujuzi wetu ni wanyumba za mapaa ya msukuma na barabara za mitaa
Bro umesahau kuwa watanzania wengi wanatumia asilimia 1 ya akili zao?.
 
Wazawa ni wezi sana na pia wavivu, visingizio kila kukicha!!!
 
Wakandarasi wazawa bado hawana vifaa vya ujenzi wanaokoteza vikukuu tu. Kulipa wafanya kazi na vibarua ni shughuli pevu hela hawana. Ujenzi hawajui wanakandika hovyohovyo tu. Ngoja wajifunze kwa wachina, wajapan na waturuki huenda wakaelewa
Wakati mwingine wakandarasi wazawa wanakosa ushirikiano wa dhati.
Kwa mfano mmoja wao kashinda tender ampe sub contractor mkandarasi mzawa mwenye sifa fulani kwenye mradi.Kwa namna hiyo watamaliza kazi katika muda uliopangwa na kuaminika kupewa kandarasi nyingine.
 
Back
Top Bottom