Mzee Kigogo
JF-Expert Member
- Jun 3, 2018
- 10,497
- 17,560
Urusi maisha magumu! Utazamia ili iwejeHivi siku hizi bado kuna watu wanazamiaga kwa meli kwenda Ulaya?
Alafu nasikia eti wa-Nigeria na ujanja wao wote wa kujaa Ulaya wameshindwa kujazana Urusi.
Hakika Russians are no joke...!!!!
Ha haaaaaa yaani ni kila mtu mjuajiSababu kubwa kunyamaza huwa hawawezi wanaweza wakajibanza kona mara ghafla bin vuu wakaanza majibizano tena kwa jazba na ghazabu nani mkali kati ya kiba na platinum mpaka wanasikika
Asante mkuu kwa kunichekesha kwa comment yakoShida ya watanzania sio wavumilivu. Akiwa mafichoni njaa ikishaanza anaanza kuzunguka kutafuta maakuli na hapo ndio hukutana na wenyewe.
Una asilia ya zanzibar au ukanda wa pwani pasi na shaka kuna vimaneno flani, unanikumbusha mwanngu Alfani yuko khazhakstan nowHao ni wa miaka hii.
Zamani kuanzia 1990s kurudi nyuma kuzamia kulikuwa kwaambatana na kufahamu lugha kama ya kiingereza ambayo ilisaidia kuelezea shida yako kwa nahodha.
Nahodha akiingiwa huruma na hapo mwazungumza mkiwa Durban, anaweza kabisa kukusaidia kwa kukupa kazi za kusafisha humo ndani ya meli.
Mkizungumza huku mkiwa ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki yaani eneo la bahari ya Hindi huwa ni shida.
Ila wale walofanikiwa kufika nchi za Italia, Ureno, Uingereza, Ubelgiji na Ireland wametumia meli moja maarufu sana ambayo sitaitaja hapa kwa sababu mbalimbali.
Hiyo meli ukiitumia uzuri basi wafika katika hizo nchi bila shida na watakiwa kufahamu tu kiasi lugha ili kuwasiliana uzuri na wenye meli.
Hiyohiyo meli wengi wa watanzania ambao walikuwa wana nia khasa ya kuzamia na sasa wapo Afrika Kusini, wameitumia na imetia nanga kwenye bandari za Beira, Maputo, Durban na Cape Town.
Umeanzisha uzi mzuri na ngoja tudadavue kidogo madaftari yetu ya zamani.
Ile messina ni ngumu mno kuitumia kutoroka nayo kwa namna ilivyojengwa mule ndani wewe kufa ni dakika sifuri tu halafu kumbuka mule ni waitaliano tupu....Nashukuru kwa Ufafanuzi na Uchambuzi wako mzuri Mkuu japo sijui ni kwanini umeamua 'Kuificha' hiyo Meli yako ya Linea Mesina kama sijaikosea.
Nipe link ya huo uzi mdau nausaka siuoniWabongo wamezidi! kuna mzamiaji alisimulia walizamia kwenye meli, usiku wakawa wanatoka mafichoni wanaenda kutafuta maakuli, walipozoea mazingira wakawa wanatafuta hadi pombe wazimue vichwa.
Wenye meli walipohisi kuna njemba ziko mafichoni wakamwaga oil kwenye eneo ambalo ni lazima wazamiaji watapita.
Kweli asubuhi wakaona kweli nyayo zenye oil zimetokea mafichoni hadi kwenye maakuli na kurudi mafichoni tena.
Mabaharia hawakuwa na kazi zaidi ya kufata nyayo zenye oil na wakawadaka wakiwa wamelewa kama wapo kwenye meli ya babu yao.
Hii meli unazamiaje milango kila kona na mbaya zaidi njia ya kwenda engine iyo kule deck ya juu na imepigwa lock ya kufa mtu hata ukisimama tu hapo kule cabin crew wanakuonaMliozamia na Linea mesina tunangoja stori jamani