Ni kwanini watu huumia wanapokuona umefanikiwa?

Ego is the Enemy

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
8,201
Reaction score
16,246
Habari zenu wanajukwaa,
Binafsi nimekuwa nikijiuliza hii hali ni kwa nini mtu unapokuwa na kitu kizuri kila mtu anakitaka awe nacho ila wengi huumia sana. siku ikitokea umekipoteza watu watafurahi sana na ilhali sio kuwa kitaenda kwa mmoja wa hao wanaochukia.
 
kwa sisi watu weusi kuna nadhalia flani tumejiwekea kwamba wote tuwe kwenye level moja ya maisha, hii ipo sana sana mitaani kwetu uko
sasa endapo wewe utachoropoka kwenye iyo level yao, hapo ndio majungu na husda kibao,
tabia hii ipo kwa binadamu wote lakini kutokana na life style zipo tofauti duniani ndio utakuta ujinga huu una base sana afrika
 
Wivu wa kijinga ndio nini dada? wivu ni wivu tu.
Kuna wivu wa kijinga na wivu wj maendeleo buana.

Wivu wa kijinga ni pale mtu anaona umefanikiwa kwa jambo au mambo yako fulani badala aulize umefanyaje, anabaki anaumia, anapita kukusema vibaya nk.

Wivu wa maendeleo ni pale mtu anapoona umefanikiwa jambo fulani hutamani na kujitahi nae kufanya hvo au hata zaid ya yako.

Wale wa kusini mwa jangwa la sahara wao wapo kwenye kundi la kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…