Wapendwa naomba kujua ni kweli fisi anajinsia mbili (jinsia ya kiume na ya kike).
Ndugu zangu habari zenu
Si kweli kuwa fisi ana jinsia mbili isipokuwa fisi tuliyemzoea aitwae spotted hyena (crocuta crocuta) jinsia ya kike ukimwona awapo mkubwa utasema ni dume kwa kuwa sehemu zake za uzazi zimechomoza nje kama uume hii imetokea kwa sababu maalumu ikiwamo kudhibiti kuzaana! nikimaanisha katka kuzaana fisi dume yampasa kuwa mpole sana na mwenye hulka nzuri ndio ataweza kumvutia jike aweze kusimamisha uchi wake ukae katika namna ambayo uume utapenya! kwa hiyo ni lazma jike aridhike na ndio maana fisi madume hawapiganii jike ila wanaonyesha matendo mema ikiwepo usafi ndio jike atapata mzuka na kuchagua bwana ambae anadhani atakuwa mwema kulinda familia!
NIMEFURAHISHWA NA MADA HII SANA NA MIMI NI MSOMI WA MASWALA YA VIUMBEPORI TOKA UDSM! NATUMAI NIMEJIBU VEMA