Ni kweli haishauriwi kutumia Coolant pelee (Antifreeze) bila kuchanganya na maji kidogo?

Ni kweli haishauriwi kutumia Coolant pelee (Antifreeze) bila kuchanganya na maji kidogo?

CHIBA One

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2018
Posts
558
Reaction score
2,093
Nimepitia makala mbali mbali kuhusu cooling system za kwenye magari,

baada ya kumpa jamaa yangu gari kwa zaidi ya miezi miwili ( nilisafiri mkoa wa mbali kikazi) Nimerudi baada ya kuchukua gari, nime experience kitu kipya, nimetoka vzuri tu lakini baada ya kutembea Km kama 10 gari ikaanza kupandisha Gauge ya temperature,

Nilianza kuhisi labda ni mambo ya themorstat ama Radiator, feni, head gasket etc,

Lakini nilipofungua bonet nilikuta coolant iko chini sana, kiasi haifiki hata Lita 1..kile ki tank cha maji ni kikavu kabisa hakina kitu.

Ikabidi nipite garage moja ya Total, nikaongeza coolant kama ltr 3..

Sasa baada ya kupitia kwenye makala online, nikaona haishauriwi kutumia coolant pekee bila Maji ambayo yalichemshwa "distilled water" kwa uzoefu wenu hii ikoje?

N.B Baada ya kuongeza coolant, Temp gauge imetulia haipandi tena.
 
Bado unatatizo , gari kupunguza coolant lita tatu kwa miezi miwili si kitu cha kawaida .
Jamaa yako ali abuse gari
Coolant huchamganywa na maji ili isipoteze boiling or cooling points za maji ambao kimsingi ndio ,mahesabu ya upoozaji yamepigiwa , unapokuwa na coolant peke yake chances are, boiling points zinaweza kuwa altered.na unaweza kuua engine kwa joto
 
Inategemea na coolant yenyewe. Soma label kwenye dumu, je imeandikwa ichanganywe na maji ratio 1:1 ama 1:4 ama coolant tu kama ilivyo.
Ooooh sawa sawa
 
Bado unatatizo , gari kupunguza coolant lita tatu kwa miezi miwili si kitu cha kawaida .
Jamaa yako ali abuse gari
Coolant huchamganywa na maji ili isipoteze boiling or cooling points za maji ambao kimsingi ndio ,mahesabu ya upoozaji yamepigiwa , unapokuwa na coolant peke yake chances are, boiling points zinaweza kuwa altered.na unaweza kuua engine kwa joto
Nafatilia mkuu kuona kama kuna leakage maana sio kawaida
 
Uzi una somo zuri, kwa wamiliki wa magari madogo, ila umekosa kuchangiwa na wataalamu wengi. Mimi siku ziku zote, nilikua najua coolant ni badala ya maji, kumbe nyingine inabidi ichanganywe na maji.

Nilichokua natofautisha ni rangi tu, kama unatumia ya rangi nyekundu usiweke ya kijani.
 
Kuna baadhi ya coolant zimeandikwa unatakiwa kuchanganya na distilled water kwa ratio fulani na nyingi zipo kwenye maduka ya uremno wa magari ila kuna zingine hakuna kuchanganya na maji ambazo mimi ndio nazotumia.
 
Nishaona washua kadhaa wakiweka maji ya povu la sabuni mbadala wa coolant kitaalam imekaaje iyo, na hao washua sio wachovu na gari si za kichovu.
 
Nishaona washua kadhaa wakiweka maji ya povu la sabuni mbadala wa coolant kitaalam imekaaje iyo, na hao washua sio wachovu na gari si za kichovu.
Maji ya sabuni na povu yanawekwa kwenye windshield washer tank....

Si kwenye radiator..
Kuna fluid maalum kwa ajili ya kuweka kwenye tank la kuoshea kioo....ila wahuni wanarahisisha kwa kuweka maji yenye sabuni.
 
Uzi una somo zuri, kwa wamiliki wa magari madogo, ila umekosa kuchangiwa na wataalamu wengi. Mimi siku ziku zote, nilikua najua coolant ni badala ya maji, kumbe nyingine inabidi ichanganywe na maji.

Nilichokua natofautisha ni rangi tu, kama unatumia ya rangi nyekundu usiweke ya kijani.
Jambo la msingi soma instruction manual ya dumu la coolant uliyonunua..

Si kila coolant unachanganywa na maji..
Kuna baadhi unaweka kama ilivyo..
Kuna baadhi unatakiwa uchanganye na maji kwa ratio maalum..
Mfano 1:1 yaani lita moja ya coolant kwa lita moja ya maji .
Maji yasiyo na madini ya chumvi au magadi yanapendekezwa hapa...
 
Maji ya sabuni na povu yanawekwa kwenye windshield washer tank....

Si kwenye radiator..
Kuna fluid maalum kwa ajili ya kuweka kwenye tank la kuoshea kioo....ila wahuni wanarahisisha kwa kuweka maji yenye sabuni.
Umenitoa tongotongo ndugu.
 
IMG_20221102_092102_904.jpg
 
Unashauriwa kila wakati kuangalia gari lako pindi unapoanza safari maana huwezi kujua kitu gani kikitokea mwisho wa safari iliyopita
 
Back
Top Bottom