Ni kweli kila jambo linalotokea ni mpango wa Mungu?

Ni kweli kila jambo linalotokea ni mpango wa Mungu?

radiation

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2013
Posts
241
Reaction score
254
Habari wanaJF,

Nimekuwa na utata ambao nimekosa majibu ya kuridhisha. Nimekuwa Nikishuhudia watu wengi kuhusisha baadhi ya matukio yanayowatokea na Mungu, kwa mfano mtu anaweza akapata ajali, kutokufanikiwa kwenye mambo yake, magonjwa, kifo nk. imekuwa kawaida watu kusema ni mpango wa Mungu.

Je, ni kweli kuwa Mungu huweza kumfanyia haya yote mwanadamu aliyemuumba kwa mfano wake? (Kwa wale wanaoamini uumbaji).

Lakini pia maandiko matakatifu yanasema "mtu ajaribiwapo asiseme najaribiwa na Mungu kwa maana Mungu hajaribiwi na uovu". Vile vile sehemu nyingine ikaandikwa "Mungu hutuwazia yaliyo mema".

Nawasilisha..
 
kila k2 kinachotokea dunian ni mpango wa mung coz mung pekee ndo mwenye uwezo wa kufanya chochte,,
 
Kwani wewe unapokosa majibu ya kuridhisha ni idea gani inakujia kwenye mind yako?
 
Noo mengine siyo mfano umechepuka halaf unapata gonjwa la ngono utasema ni mpango wa Mungu au unaendesha gari uku umelewa halaf unasababisha ajali utasema uo ni mpango wa Mungu mengine ni watu wenyewe wanajiletea
 
Mi nahisi Mungu katupa akili na uwezo wa kufanya maamuz wenyewe. Kwa hiyo kila kinachotokea kwenye maisha inatokana zaidi na interactions zetu sisi wenyewe wanadamu.

Huwezi kuwa mzinzi afu ukapata gonjwa afu unasema ni mpango wa Mungu.

Kama upo chuo husomi afu ukadisco huo hauwezi kuwa mpango wa Mungu.
 
hiyo kauli ya dini inapingana na hi I hapa....kila jambo liwe zuri au baya kalichuma kwa mikono yake,..interactions zetu na maisha yetu ndio yatayo determine matukio yetu hapa duniani...maidha yetu Je ni mema kiasi gani au yanauovu kiasi gani...hata ivo ujuzi wa mungu umetangulia kujua kila MTU na matendo yake yapoje na yatakuwaje na Mungu hubaki kuyatathimini ili yapite ktk proper channel.... hata hivo kauli ya kusema mwanadamu kaumbwa kwa mfano ea Mungu inawalakini huwenda waliotransalte bible walikosa kiswahili chake vizur
 
Noo mengine siyo mfano umechepuka halaf unapata gonjwa la ngono utasema ni mpango wa Mungu au unaendesha gari uku umelewa halaf unasababisha ajali utasema uo ni mpango wa Mungu mengine ni watu wenyewe wanajiletea

Mpango wa Mungu ni kama upi?
 
Lowasa ni mpango wa Mungu
 
Unajua Mungu alipotuumba, alitupatia na uwezo wa kutawala mazingira. Hivyo, kuna ambayo inakuwa mpango wa Mungu tuyapitie, lakini mengine, kutokana na ujinga wa kutoyatawala mazingira, wanadamu tunapatwa na mabaya na mwisho tunamsingizia Mungu.
 
Jiulize,tafakari na chukua hatua,wana wa Israeli wakati wako Misri waliteseka mateso ya kufa mtu lakini ilikuwa ni mpango wa Mungu kuwandaa kwa ajili ya nchi ya ahadi.Kwahiyo mpango wa Mungu unaweza kuwa machoni ni wa maumivu lakini una lengo zuri sana na unaweza machoni ukaonekana mzuri na bado pia ukawa na lengo zuri.Mfano ili mwanao aweze kufanikiwa katika maisha yake jambo linaloweza kupelekea hata kuwa mchungaji mwenye mafanikio makubwa na kuwakomboa watu wengi waweze kumrudia Mungu kama akina Joe Davie,mzee wa Upako,Mwingira,TB.Joshua nk inabidi wewe ufe ili mtoto wako ajikite kwenye maswala ya Mungu kwani yawezekana uwepo wako Duniani unakuwa kikwazo kwa hilo kutimia.
 
Ukitokewa na baya ni mipango ya Mungu ipo siku yatapita. Ukitokewa na mazuri, unajisifia wewe noma. Binadamu ndiyo tulivyo.
 
Kwanini wengine aje kuwaingiza peponi/mbinguni na wengine motoni then?
Ikiwa kila kitu kapanga mwenyewe?

mwanzon shetan alikuwa malaika, baada ya kumkosea mung ndo akalaniwa hapo ndipo akamwahd mung kwamb atawajarb waja wake,, mungu akamwambia atakaye kufwata wew utakuwa naye moton,,,, linapo tokea jamb baya ni shetan ndo anamjarb mwanadam lakn shetan kama shetan hawez fanya haya ikiwa mungu hajaafik,,, unapokubar kuingia kweny mtego wa shetan na kuacha kumuomb mung ndipo hapo jamb baya hukukuta,,,
 
Jee kuafik ni kupanga?

Katika mipango ya Mungu shetani anahusika vipi?
 
Back
Top Bottom