Ni kweli kwamba nnauvimbe kwenye ovary?, na je nifanye nini?

minagirl

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
269
Reaction score
35
Poleni na majukumu,

naomba ushauri juu ya tazizo hili ambalo mbali na kunitesa lakini pia linanipa mawazo kwani sijielewi mwenzenu.
Nilianza kuugua tumbo tangu december mwaka jana, nilikua nikipata maumivu upande wa kulia kwa chini lakini haikuwa freequenty, nikawa napotezea, siku moja nikamuuliza doctor mmoja akaniambia kama haliumi mara kwa mara itakuwa ni mayai ya uzazi.nikaridhika kwa vile nilikua nahisi maumivu marachache sana kama mara tatu kwa mwezi.

siku zilivyozidi kwenza maumivu yakawa yanaongezeka hatimae nikawa najisikia maumivu karibu kila wiki, maumivu yakawa makali na sasa nikaanza kujisikia kama kuna kitu kianichoma maeneo hayo( sehemu ya chini ya tumbo upande wa kulia) nikaona sasa lazima kutakua na tatizo.

nilitinga hospitali(sitaitaja jina) kwa mara ya kwanza nikamueleza doctor jinsi ninavyojisikia, aliniandikia kupima utrasound, nikapima na nikaambiwa kuwa nna uvimbe kwenye ovary ya kulia, nikapewa vidonge nikaambiwa nitumie then baada ya mwezi nikachekiwe tena kama utakuwa unapungua ili niongezewe dawa au kama utakuwa unaongezeka nifanyiwe oparesheni.

nilianza dozi na hapa ndipo nilipoanza kujisikia maumivu kiasi cha kutaka kukata roho, nilianza sasa kusikia uzito, vichomi na maumivu makali maeneo hayo. nilikua nikiishiwa kabisa nguvu, ikabidi nirudi hospitali, nikamueleza doctor, doctor akanishauri ninywe maji mengi na chakula cha kutosha.

baada ya muda nikaanza kusikia ganzi kwenye mguu wa kulia, nikaona uzito unaongezeka maeneo hayo, kwa vile nilikuwa nimemaliza dawa nikapata wazo la kwenda kupima hospital nyingine ambako ndipo nilipopta utata juu ya ugonjwa wangu na mpaka sasa sielewi cha kufanya.

nilivyofika hospitalini hapo( jina nnalihifadhi) nilimuelezea doctor tatizo langu na kumuonesha vyeti na dawa nilizowahi kuzitumia, nae aliniandikia kupima utrasound na vipimo vingin karibu vyote, majibu ya utrasound yalitoka siku ileile lakini ya vipimo vingine niliambiwa niende kesho yake kwa vile muda ulikuwa umekwisha, nilirudi kwa doctor na kama mnavyojua miandiko na lugha zao za kiganga mm sikuelewa kilichoandikwa. dactari aliniambia uvimbe umeongezeka kwa hiyo niende siku inayofuata ili anifungulie fail ili niweze kuonana na specialist.

nilipoenda kesho yake sikumkuta yule daktari alienihudumia siku iliyopita, nikaingia kwa dactar mwingine, nikamueleza matatizo yangu, alipoangalia picha ya utrasound akaniambia mbona hauna uvimbe? watu wengine mnapenda uvimbe eeh, nani kakwambia kuwa unauvimbe? nikamwambia dactar aliyepita alikua ameniambia kuwa nna uvimbe,haata hivyo nilishawahi kuambiwa hivyo katika hospital nyingine, dactari akasisitiza kuwa sina uvimbe ila nna ugonjwa kwenye ovary.akaniandikia dawa nikatoka ila sikuridhika. nikarudi kule nilikopimwa nikamuuliza yule mbaba alienipima, akanijibu kuwa kazi ya kunieleza naumwa nini sio yake ni ya dactar, nilimueleza kuwa nimepata utata kwa madactari kwani mmoja kaniambia nna uvimbe wakati mwingine kaniambia sina uvimbe.

Baada ya kumuomba sana yule baba aliniambia binti unauvimbe, akanionesha kwenye picha na pale alipoandika na sentimita za ukubwa wa uvimbe wenyewe ila akaniambia kuwa haujafikiwa kupasuliwa,

nikaenda kuchukua dawa nilizoandikiwa na yule dactar, cha ajabu dawa zile ndo zilezile nilizokuwa nimeandikiwa katika hospitali ya kwanza ambayo niliambiwa nnauvimbe na sasa huyu aliyeniambia kua sina uvimbe kaandika dawa zilezile, nikarudi tena kwa yule dactari, nikamwambia dawa zile nilishazitumia, nikamuonesha na chet, akasema wale walinipa dozi ndogo. akaniambia nikameze then after two weeks nirud tena pale.up to now naendelea na dozi.

kinachonipa utata mpaka muda huu:
1.sielewi kama nna uvimbe tumboni au sina
2. kama sina kwanini dawa nilizopewa na yule alie niambia nnauvimbe na alieniambia sina uvimbe zifanane?
3. kwa nini dactar mmoja aniambie nna uvimbe na mwingine aniambie sina uvimbe kwa picha moja na hospitali moja?
4.na kama kweli sina inawezekana nnaumwa ugonjwa gani wa dizaini hii? maana alieniambia sina hakunifafanulia
5. kama kweli nnao sitokuwa nimechelewa kwa muda wa hizi wiki mbili nilizoambiwa nitumie dawa?
6.nifanye nini? maana sielewi ingawa nameza dawa.

naombeni ushauri wenu please! nimebaki dilema.
asanteni.
 
umepewa dawa ya Aina gani?inaonekana una ovary cyst na unapewa dawa za kutibu cancer!
 
mimi49, nimepewa sypro za wk mbili, doxaslyn nazo za wiki mbili pamoja na flagyl za wk moja.
 
Any of the following can cause Right sided lower abdominal pain
Appendicitis/Abscess
Period/pid/Pancretitis
Endometriosis/ectopic
Neoplams
Diverticulitis
IBS
Cyst /crohn's d'se
Intususception
Torsion of the ovary
IBD
Stones in the kidney

These are the only cause of right sided lower abdominal pain

most likely you have PID/ABSCESS sina historia nzuri ku specify ni nin kat ya hivyo
Ovarian cyst/ovarian tumour can also be! Bt they are not associated with menstrual irregulaties though they can present with severe right lower abdomen pain that radiates to the lower limb, this can also be the cause of u'r problem but we dont treat this with antibiotics and is also very common among young women.
contact me for free i might need more history for further advice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…